
Wakati tunaongea-tukakubaliana tuipige namba hiyo ili tumsikilize vizuri mtu anayejiita Mganga, ambapo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa. Mwisho wa siku alituma tena ujumbe akisema "Naomba unitimie sms ndg yangu niko kikaoni"
Palepale tukavuta hisia na jamaa zangu wale ofisini ambapo miezi kadhaa iliyopita, namba hiyo hiyo iliwahi kutumiwa kutapeli waandishi na wahariri fulani wa vyombo vya habari na hata sisi kwa utatu wetu (tuliokuwa pamoja ofisini Jumamosi) iliwahi kututapeli namba hiyo, lakini hatukuuingia mkenge huo na taarifa kuhusu namba na mhusika tulifikisha katika kituo cha polisi cha Msimbazi ili zifanyiwe kazi. Kinachoonekana ni kuwa mmiliki wa namba hiyo ambaye uchunguzi wetu wa awali baada ya tukio la kwanza, ni mwanamke maana kumjjua mtumiaji wa namba ya simu siku hizi ni rahisi, iwapo unaweza kumtumia tu hata kama ni sh. 200 kwa mtandao wowote jina lake litakuja katika meseji utakayojibiwa. Polisi waliahidi kuwa watafuatilia na mhusika atafikishwa mbele ya vyombo vya dola.
Wadau nimeileta kwenu namba hii ili muwe makini. Nchi yetu kwa sasa imegubikwa na wizi wa kutisha wa mitandao, kuanzia ile ya mawasiliano ya kompyuta hadi simu ingawa wanaotapeliwa wengi hawasemi tu --
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments