[wanabidii] Gesi ya Mtwara: JK na Muhongo wameshindwa kazi!

Friday, January 04, 2013
Wanabidii,
Nilisikiliza kwa masikitiko na majonzi hotuba ya mwaka mpya ya Rais JK
na juzi nilisikiliza maelezo ya Prof Muhongo kuhusu gesi ya Mtwara.
Wote wawili kwa bahati mbaya wameshindwa kujieleza kwanini watu wa
Mtwara wanapuuzwa. Hii inatokana hasa juu ya ubovu wetu wa kumiliki
mali zetu za asili na wizi wetu wa kupeleka pesa Switzerland. Watu wa
Mtwara hawapo tayari kujitoa muhanga ili mafisadi wazidi kupeleka pesa
zetu Switzerland.
Kulinganisha sisal, kahawa, tumbaku na gesi ni kuishiwa na akili,
kwasababu huwezi kabisa kulinganisha upatikanaji wa mazao hayo na
gesi.
Kama ingelikuwa wananchi wa Mtwara kila mmoja na canisters zake
anakuenda shambani kuvuna gesi na baadae kuiuzia serikali hapo
ingelikuwa suala jengine. Lakini gesi haipatikani hivyo.
Tunangojea na huko Visiwani ili tuone suala hili watalimudu vipi,
kwasababu gesi nyingi inasemekana ipo Pemba. Kama na wao wataichukuwa
kuipeleka Zanzibar na kuwaeleza wananchi wa Pemba kuwa mbona karafuu
wakifanya hivyo itakuwa pia ni kupungukiwa na akili.
Huko nyuma Tanzania ilikuwa haina gesi na kwahivyo hivi sasa ni lazima
iwekwe mikakati mipya na formula mpya za ku-deal na products kama hizi
ili wananchi wa maeneo husika wafaidike pamoja na nchi nzima na sio
kila siku tunasema mbona sisal, kahawa, tumbaku ilikuwa hivi au vile.
Tukifanya hivyo tutakuwa sawa na yule kipofu aliemuona punda siku moja
na baadae kila kitu akawa analinganisha na punda tu.
At present, it doesn't seem that the govenement is taking serious
steps to study this issue. Kama wahenga wanavyosema: kama hutajenga
ufa basi mwishowe utajenga ukuta.
Kwa maneno ya JK na huyu bwana Muongo, Watanzani tujiandae kuja kujenga ukuta!

Geo.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments