[wanabidii] CUF yajichanganya kuhusu sera ya Muungano

Sunday, December 30, 2012
Ndugu Wanabidii,

Bila shaka baadhi mlipata fursa ya kutazama kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa na kituo cha televison cha Star TV. Yalizungumzwa masuala mengi na yenye tija lakini nitapenda kugusia suala la Muungano.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF ndugu Julius Mtatiro akijibu swali la mtazamaji mmoja kupitia mtandao wa Jamii Forums aliyetaka kujua kama CUF kinaunga mkono hoja ya mkataba au la. Ndugu Mtatiro alibabaika sana katika maelezo yake na katika kubabaika huko aliongeza mashaka zaidi juu ya nini hasa sera ya chama chake kuhusu Muungano. Mwisho akasema chama chake kinaunga mkono serikali tatu na kiujanjanja akajaribu kuitetea dhana ya mkataba kama vile ni haja ya makubaliano hivi ya namna ya kuendesha hizi serikali tatu na mwisho katika namna inayoonesha kumuogopa Katibu Mkuu wake ambaye moja kwa moja ametangaza hadharani tena kwenye jukwaa la kisiasa kuunga mkono mkataba akatupia mzigo kwa viongozi wa juu labda watalisemea zaidi.


Katika maelezo ya Mtatiro nimepata mambo mawili; moja, kwamba Mtatiro binafsi haamini na hakubaliani na hoja ya mkataba lakini anashindwa kusema hadharani na Pili, kwamba CUF kama chama hawajakubaliana au hawakubaliani juu ya jambo hili. Kwa mujibu wa watetezi wa mkataba, Zanzibar inapaswa kuwa na mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa ikiashiria vivyo hivyo kwa Tanganyika. Ukishakuwa na Serikali ya Zanzibar na Tanganyika zenye mamlaka kamili utahitaji serikali ya tatu ya Muungano ya kazi gani na itayatoa wapi mamlaka yake wakati kila nchi ina mamlaka yake kamili mikononi mwake? Huhitaji kuwa Albert Einstein kujua kuwa hawa wanataka kuvunja Muungano. Kimsingi watetezi wa mkataba wanataka kuvunja Muungano lakini wameamua kupitia njia yenye kona nyingi kama sehemu ya kuhadaa wananchi hasa wasiotaka Muungano uvunjike.

Nadhani ni muhimu CUF kikatolea ufafanuzi juu ya sera yake ya Muungano la sivyo itaonekana kuna vyama viwili ndani ya kimoja, kimoja kikitaka serikali tatu na kingine mkataba. Kutokuwa na sera inayoeleweka kutawachanganya watanzania na mwisho wakiacha kuwachagua mtalalamika kura zenu kuibwa au tumekosa kura kwa sababu pale wanaishi watu wengi kutoka bara!

Namuunga mkono Zitto kuhusu mantiki ya Muungano. Kwamba tunaweza tusiwe na kitu kizima kama jiwe la kulishika mkononi na kusema hiki au huu ndio faida ya Muungano. Lakini ile heshima tulioujenga kwa Afrika kutofungwa na mipaka ya kufikirika ya kikoloni ni kitu kizito sana. Ni jambo la ajabu sana kwamba tunaheshimu sana hivi vinchi vya kikoloni ( call them Bismarck states), Tanganyika na Zanzibar kuliko nchi iliyoundwa na waafrika wenyewe( Tanzania). Pia nakubaliana naye kwamba ukiruhusu sehemu moja ya nchi kujimega unahalalisha mmomonyoko endelevu maana hakutakuwa na hoja ya kuwazuia wengine wasijitenge.

Nafikiri ifike mahali kujadili suala la kuvuruga Muungano iwe ni mwiko kama ilivyo mwiko kwa watoto kujadili kuvunja ndoa ya baba na mama yao eti kwa kuwa walikosea taratibu za kuchumbiana!

Nawatakia mwaka 2013 wenye baraka tele!
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments