Moja ya kazi ambayo CCM na washirika wao wa kisiasa nje ya chama
hicho, wamekuwa wakijaribu kuiaminisha jamii ya Watanzania kuwa
wanaiweza ni kusema uongo. Kudanganya. Na kwa siku au miaka ya hivi
karibuni, hasa kwenye mfumo wa kisiasa wa vyama vingi, wamefikia hatua
ya hatari zaidi. Wanaweza kusema lolote, wakafanya chochote, almuradi
kukidhi political expendiency yao. Na mara nyingi huwa ni hoax au
quick fix, hata kama taifa na watu wake wataangamia.
Mfano dhahiri ni elements za udini na ukabila zilizoanza kujionesha
kwa muda fuoani sasa. Lakini hasa zikianza wakati ule CUF kilipokuwa
kikikubalika miongoni mwa jamii kubwa ya Watanzania. Wakati kulipokuwa
na ombwe, zikafifia. Zimerudishwa tena na CCM baada ya Watanzania
wengi kujibainisha na CHADEMA kama tumaini lao jipya.
Nani asiyejua kuwa kwa sasa nguvu kubwa ya Watanzania juu ya matumaini
ya mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala imelalia kwa CHADEMA?
Kiasi cha kukaribia kuvunja mizani ya upimaji wa mizania ya kisiasa,
linapokuja suala la kulinganisha CHADEMA na CCM?
Wakati taifa likiwa kwenye mtanziko wa elements za kijinga na
kipumbavu, zinazolazimishwa kuwepo, za udini na ukabila, CCM
wameendelea kuchochea kuni. Wakati wanachochea wengine wetu kwa kujua
au kutokujua, tumejitahidi kweli kusogeza kuni zaidi, lakini walio
mabingwa wanasogeza na petroli kabisa.
Chochea kabisa. Choma taifa. Unguza ikibidi. Lipua nchi, lipua. Majivu
yatabaki, eti ili kuokoa CCM ipone dhidi ya CHADEMA. Isiondolewe
madarakani.
Matokeo ya kuchochea huko ni kama moja ya thread iliyoanzishwa hapa JF
ikieleza kile kinachodaiwa kuwa safu ya viongozi wa CHADEMA matawi ya
vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.
Nitaweka some facts hapa kuonesha uongo huo wa hatari kabisa wa CCM
kulazimisha watu wajadili ukabila. Na kwa sababu natambua msukumu huo
wa kuwataka watu wadumae akili wajadili dini zao na kabila zao kama
vile ndiyo sababu ya gharama za maisha kupanda, kuongezeka kwa
umaskini, ukosefu wa maisha bora, kuminywa kwa haki za binadamu,
sitaingia huko...
Hapa chini nitaweka majina baadhi ya viongozi wa matawi ya vyuo vikuu.
Usiku nimelazimika kufanya kazi ya hovyo kabisa, kumuuliza mtu
anatokea sehemu gani ya nchi na kabila lake, kwa ajili ya kujenga
hoja. Lakini ili hoja ibaki na mashiko sitaingia kwenye mtego ambao
CCM wanataka kila mtu aingie, kujadili kabila au dini ya mtu badala ya
sifa zingine za msingi katika uongozi, kama uwezo na uadilifu.
Kosa la kwanza kabisa katika thread ile iliyoanzishwa makusudi
kuendeleza propaganda chafu za ukabila dhidi ya CHADEMA ni kusema kuwa
Viongozi hao 'waliopangwa' watakisimamia chama kwa miaka 5. This is
rubbish.
Hivi mwanafunzi yupi anakaa chuoni zaidi ya miaka 5! Ukweli ni kwamba
uongozi wa CHADEMA katika matawi yote ya vyuo vikuu huchaguliwa kila
baada ya mwaka mmoja. Na hili linaeleweka kwa kila mtu anayejua nature
ya masomo ya chuoni au hata kuanzia shule za kawaida, ambapo kila
mwaka lazima kuna watu wanaondoka baada ya kuhitimu.
Tunakuja kwenye majina. Hakuna haja kabisa ya kutaja kabila la mtu
hapa, wala anakotokea. Maana hazikuwa sifa zao wakati wakiomba
kugombea na baadhinyao wakachaguliwa miongoni mwa wengi waliojitokeza.
Umuhimu wa kuweka rekodi sawa hapa unatokana na ukweli kuwa katika ile
thread nyingine, umesemwa uongo kwa kutaja majina ya watu kuwa ni
viongozi wa chama katika matawi ya vyuo vikuu wakati si kweli, huku
viongozi halisi wakiachwa.
Chuo Kikuu MZUMBE
Mwenyekiti ni Roda Edward
Katibu ni Bariki Mwakibete
Chuo Kikuu cha UDOM
Mwenyekiti ni Nchimbi Method
Katibu ni Malale Sende
Chuo Kikuu cha Mwenge
Mwenyekiti ni Abel Dendwa
Chuo Kikuu cha SAUT
Mwenyekiti ni Patrobas Paschal
Katibu ni Makoko Obadia
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)
Mwenyekiti ni Paul Ndeje
Katibu ni Masuala Masaga
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph - Thobias Leizer
Chuo Kikuu cha Jurdan - Newton Chamkongo
Chuo cha Mtakatifu John
Salvatory Sege
Leiza Maige
Chuo Kikuu Kishiriki DUCE - Atupele
Watakaotaka facts zaidi kwa ajili ya constructive criticism and
critiques waseme tuwaongezee. Watakaotaka kuendelea kujadili ukabila,
udini, rangi au eneo analotoka mtu kama vitu vya msingi sana kwao
katika kujadili viongozi bora waendelee.
Wengine tutajadili sifa za muhimu za kiongozi bora ambaye inawezekana
akawa hana dini kabisa au hajui mlango wa msikiti au kanisa mara ya
mwisho ulibadilishwa lini au huenda hata kabila lake halijui.
Haya tunayoyashuhudia sasa ni mwendelezo wa matokeo ya chama au wana
CCM wanaotapata na kupigania roho zao, wakiliona anguko kuu. Baada ya
kuona kimeshindwa kusimamia misingi ya utaifa na hasa misingi ya amani
na utulivu, CCM wako katika hatua za mwisho mwisho ambazo watawala
wengi hupitia na wako tayari kusema au kufanya lolote...lolote lile,
ikiwemo assassinations (za aina zote, ikiwemo character)
Amani na utulivu, Mwalimu Nyerere, in one of his radical speeches,
anasema vilijengwa juu ya misingi ya haki na matumaini (then, based on
Azimio la Arusha). Kama watu hawaioni haki na matumaini hawana,
usitegemee amani na utulivu na Watanzania watakuwa wapumbavu
wakiendelea kukubali kutawaliwa katika hali ya namna hiyo.
Wote wangekuwa ni Wachagga
Nataka tu kuweka rhetoric questions hapa. Kwani wangelikuwa wote ni
wachaga kulikuwa na tatizo gani? Wapiga kura wote walikuwa wachaga?
Wachaga hawana haki ya kuchaguliwa na kuchagua? Hivi wakikutana watu
wengi kuchaguana wakamuona Mchaga au mwislamu au mkristo au mpagani,
ndiye mwenye sifa na anafaa kuwa kiongozi wao kati ya wengi waliopo ni
nongwa? Ni tatizo? Where does this character assassination comes from?
So what?
Inawasaidiaje hawa watawala waliochoka? Je wananchi waliochoka zaidi
kutokana na maisha magumu badala ya maisha bora wanawaelewa watawala
wanavyowawekea pilipili machoni na kuwaongoza shimoni?
Mambo yameanza kuwa mabaya, nasikia tetesi kuwa imefikia mahali ndugu
zetu hawa wanalazimika kuficha majina yao wanapotafuta kazi. Hawasemi
tena au kutumia majina yao ya kiukoo kama walivyopenda huko nyuma. No
justice, no hopes, CCM inaua taifa hili. Mtambue hao hao mnawaambia
chama cha kikabila hao hao mnawaambia chama cha kidini, mnasahau kuwa
miongoni mwa waislamu kuna wachaga na miongoni mwa wakristo kuna
wachaga, so as to every religion and tribe, ndani ya nchi hii.
Lakini juu ya yote, wachaga ni akina nani hasa? Hivi kuna mtu amezuiwa
kuwa na aggressivennes kama ya warombo, wamachame, na wakinga na
wengine wa namna hiyo katika kutafuta mafanikio kupitia biashara,
kutokana na nature ya mazingira waliyokulia?
Watu wanahitaji haki na matumaini kutoka kwa viongozi wao si umahiri
wa kutunga vitu na kuligawa taifa vipande vipande kuiokoa CCM.
Wanataka badala ya kujadili kushindwa kushughulikia ufisadi, kujivua
gamba, maisha magumu na madai ya makundi mbalimbali ya kijamii kudai
haki na uwajibikaji, tuanze kujadili dini, kabila, ukanda na.
Hawatafanikiwa.
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/356884-facts-juu-ya-uongozi-wa-chadema-vyuo-vikuu%3B-kusema-uongo-ni-kazi-wanayoiweza.html
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments