Wazalendo,
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa taarifa ya awali kuwa TPN inakusudia
kuandaa siku ya wanataaluma Tanzania.
Tunatarajia itafanyika mwisho wa mwezi desemba 2012 hapa jijini Dar Es
Salaam, tarehe kamili na ukumbi tutawajulisha baadae mara baada ya taratibu
za awali kukamilika .
Siku hii kutakuwa na mambo yafuatayo:
1. Mkutano wa mwaka wa wanachama wote ( wanachama wetu wote wa ndani na
walio nje ya nchi mnakaribishwa sana kushiriki maana wengi kipindi hiki
wanakuwa likizo, wale mnaopenda kujiunga na TPN pia karibuni)
2. Kongamano la wanataaluma wote kujadili mambo mbali mbali kuhusu
Taifa letu
3. Tuzo za mwaka kwa wanataaluma walio ndani na nje ya nchi waliofanya
vizuri katika fani zao (Tiba, Elimu,Sheria, Sayansi na Teknolojia, Habari,
Uchumi, Sanaa, Siasa n.k)
4. Hafla ya kumaliza mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka mpya 2012
Nawakaribisha wote tujumuike na kushiriki kikamilifu kwa hali na mali katika
maandalizi ili kufanikisha siku hii kubwa ya wanataaluma Tanzania.
Maoni na ushauri vyote vinakaribishwa, mnaweza kuwasiliana na walitajwa hapo
chini.
Nachukua nafasi hii kuwaomba wadau wetu wote mtakaopenda kushirikiana nasi
katika kufanikisha siku hii kwa kudhamini au kufadhili matukio ya siku hii
muwasiliane nasi .
Nawatakia wote kila la heri.
Phares Magesa,
Rais- TPN,
+255 (0784/0713/0767) 618 320
magesa@hotmail.com
Richard Kasera,
Makamu wa Rais- TPN
+255 767 777151
rkasesela@gmail.com
Mhe. Bi. Janet Mbene (MB),
Katibu Mkuu - TPN
+255 784 596 444
maorchid@gmail.com
Gervas Lufingo
Mhazini- TPN
+255 784 482597
nasemaasante@yahoo.com
Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN),
Url: www.tpntz.org
Email: president@tpn.co.tz
----------------------------------------------------------------------------
----------------------------------------