Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Said Mwema, amefanya mabadiliko kwa
baadhi ya makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi.
Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani
SACP Ernest Mangu anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
kuziba pengo la marehemu ACP Liberatus Barlow, ACP David Misime
aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke kwenda kuwa Kamanda wa
Polisi mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya SACP Zelothe Steven
anayestaafu. Vilevile, aliyekuwa kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege
ACP Ulrich Matei anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani.
Aidha, wengine ni kutoka Makao Makuu ya Polisi na Makao Makuu Idara ya
Upelelezi ambapo ACP Engelbert Kiondo kutoka makao makuu Idara ya
Upelelezi anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, ACP Rashid
Seif kutoka Makao Makuu ya Polisi Kwenda kuwa Kamanda wa kikosi cha
Tazara, ACP Deusdedit Kato kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa
Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, ACP Shaban Hiki kutoka Kamanda wa
Kikosi cha Ufundi kwenda Makao Makuu ya Polisi na ACP Lucas Mkondya
kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Kikosi cha
Ufundi.
Mabadiliko hayo pia yamehusisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa kikosi
cha Usalama Barabarani ACP Johansen Kahatano anayekwenda kusimamia
Mradi wa SMARTER Traffic ambapo nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa
RTO mkoa wa Pwani ACP Swalehe Mbaga. Uhamisho huo pia umewahusisha
baadhi ya Wakuu wa Operesheni wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi vya Kutuliza
Ghasia vya Mikoa, Wakuu wa Polisi wa Wilaya na Wakuu wa Upelelezi wa
Wilaya.
Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo
ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-ASP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments