[wanabidii] Kambi ya Taifa ya Kikapu kuzinduliwa 07/11/2012

Tuesday, November 06, 2012

 

Taarifa kwa Umma,  tarehe 06/11/2012

  

Kambi ya Taifa ya Kikapu kuzinduliwa

 

Tuna Furaha kuwatangazia kuwa Kocha wetu wa timu ya Taifa ya Kikapu Jocuis Sconiers amabye ni Kocha Msaidizi wa Kocha Mkuu Albert Sokaistis amewasili awali na kambi ya timu ya Taifa imeanza toka jana.


Kocha Mkuu Sokaitis atakuja nchini baadae kuungana na Sconiers ili kuendeleza mafunzo haya katika mpango  wa maendeleo ya kikapu wa miaka 4, ambao tutakuwa tunaufanyia tathimini kila baada ya miaka 2.


Awamu hii ya kwanza ya mpango wa mafunzo unadhaminiwa na watu wa Marekani kupitia ubalozi wao hapa Tanzania, tunawashukuru sana watu wa Marekani.

 

Afisa wa mambo ya Umma wa ubalozi wa Marekani nchini atakuwa mgeni rasmi katika kufungua kambi hii ya timu ya Taifa , uzinduzi huo utafanyika jumatano  tarehe 07/11/2012 katika viwanja vya Don Bosco saa 4.30 asubuhi. 

Tunaomba wadau wote mtuunge mkono kwa hali na mali kufanikisha mpango huu wa mafunzo kwa timu ya Taifa na kwa makocha wetu wazalendo kwa faida ya vijana wetu na Taifa letu.

 

Mungu Ibariki Tanzania

 

PHARES MAGESA

MAKAMU WA RAIS-TBF

+255 784 618320

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments