Jana Rais Joseph Kabila wa DRC amezungumza na waandishi wa habari kutoka Tanzania, Ikulu ya jijini Kinshasa ambapo pamoja na mambo mengine, amesema ndoto yake kubwa ni kuiona DRC inakuwa taifa lisilokuwa na vita hasa upande wa mashariki mwa nchi hiyo. Akasema vita kwenye eneo hilo dogo la DRC inachochewa na waasi wa jeshi la serikali wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda. Hata hivyo akasema serikali yake inatumia njia ya kidiplomasia kupata suluhu ya mzozo huo na kwamba ikishindikana, watafungua njia ya mazungumzoa ya kisiasa na hatimaye kuliandaa jeshi imara la DRC, ili kurejesha amani katika eneo hilo. Msingi alisisitiza matumizi ya mazungumzo. Alipoulizwa kuhusu kinachomnyima usingizi katika utawala wake, akasema ukosefu wa amani kwenye eneo dogo Mashariki mwa DRC na umasikini wa watu hususani vijana 'vinamkosesha usingizi', hivyo ameweka mkakati wa kisheria na uwajibikaji kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinapata suluhu ya kudumu. Kwa vile nilihudhuria press conference hiyo, nitatoa dondoo ili wenye hostoria na maoni tofauti kuhusu DRC wajadili. |
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments