[wanabidii] Fw: Muhimbili University New Campus

Monday, November 26, 2012





Wapendwa huu mjengo wa quality!
 
Michoro ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila iliyo katikati ya Wilaya za Kisarawe Mkoa wa Pwani na Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam ambayo ni sehemu ya Hospitali kuu ya Muhimbili inajengwa kwenye eneo la ekari 3800 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya wapatao 15,000 kwa mwaka, na pia itakua sehemu ya kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na ya kawaida nchini. 
Ujenzi wa Hospitali hii, ambayo pesa ya ujenzi wake imeshapatikana, unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada ya ujenzi kuanza. Tayari wataalamu na wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika kampasi ya Mloganzila wameshaanza mafunzo ndani na nje ya nchi. Mara hospitali hiyo kubwa na ya kisasa itakapokamilika itakua na uwezo wa vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita (600). Hii ni mojawapo ya juhudi za serikali ya awamu ya nne katika kuhakikisha nchi inaondokana na adha ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Visit a youtube site for more audiovisual
http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=DLzsq3JiUYA


Share this :

Related Posts

0 Comments