Unapoenda kutoa fedha katika benki ya NMB tawi la Mbagala Zakhem
unakaribishwa na foleni ndefu. Foleni hizo huwa za aina mbili moja ya
kuingia ndani ya benki ambayo inaanzia ndani na ya pili ni kwenye
mashine ya kutolea fedha, sijui niseme kijiji chetu cha Mbagala
watu wana pesa nyingi au la?
Hali hii inafanana pia kwenye matawi mengine ya benki hii ambayo
inajitapa kuwa ni benki ya makabwela,yaani akina yakhe
wakimaanisha kuwa ni ya watu wa kima cha chini. Pengine wito huo
wa benki ya makabwela unafanana na adha wanayopata wateja wake kwa
kupanga foleni ndefu , huduma kuchelewa, mashine kukorofisha hasa
wakati wa mishahara.
Mashine za kutolea pesa zimekuwa na desturi ya kutofanya kazi.
Sasa,wageipa jina kuwa NMB ni benki ya matajiri nadhani huduma zake
zingelingana na hali hiyo lakini kwa makabwela yaani sie pangu
pakavu tia mchuzi, tabu ni sehemu ya maisha.
Nakumbuka ijumaa nikiwa tawi la NMB Mkwawa nilikaribishwa na
foleni kubwa huku mashine hizo zikiwa likizo kufanya kazi.
Kilichonisikitisha leo si foleni ya NMB tawi la Mkwawa mjini
Iringa bali ni tatizo la mashine ya kutolea pesa ya tawi la
benki hiyo iliyopo Mbagala Zakhem ambapo huweza kuona vizuri
maandishi ya mashine hiyo kutokana na jua. Ata wakati mwingine kama
jua halipo, hali hii inatokana na mashine hiyo kuwa na giza. Kwa
wale wenye macho manne au wale macho ya kizee kama yangu tambua
kuwa unaweza kusikia kuwa kadi yako imebaki ndani ya mashine
kutokana na kubonyeza sehemu isiyo sahihi.
Jamani NMB na hasa NMB tawi la Mbagala Zakhem wekeni kibanda cha
kuzuia mwanga angalau wateja wenu waweze kupata huduma vizuri au
kama mashine hiyo inaweza kuongezewa mwanga basi hilo lifanyike
kuwaondolea kero wateja wenu.
Unaweza kuona kuwa mteja huyo kwenye picha ya kwanza kajaribu
kukinga mwanga wa jua kwa mkono angalau aweze kubonyeza shemu sahihi.
Wasalaam Adeladius Makwega, kutoka kijijini kwetu, Mbagala.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments