Na Maggid Mjengwa,
ASKOFU Desmond Tutu alipata kuyasema haya;
" Kuna tofauti ya kimsingi kati ya kuwa huru na kuwa katika hali ya kukandamizwa. Kuwa huru ni pamoja na kupata huduma za msingi za kijamii; kuwa na ajira, maji ya bomba, umeme, makazi bora na huduma za msingi za afya. Kuna maana gani basi ya kuwa huru wakati ubora wa maisha ya watu haujaimarishwa? Kama sivyo, hata kura nazo hazina maana yeyote!" – Desmond Tutu ( William Gumede; Thabo Mbeki And The Battle For The Soul Of The ANC, Uk. 67)
Na mwanafasihi Mtanzania Profesa Kezilahabi anayesema haya: " Siku hiyo ikifika utaona ishara itakayokuongoza. Utakapofika pale ambapo kila binadamu lazima afike utajua hukukosea; kwani njia ya kwenda huko inajulikana kwa wote na inakwenda moja kwa moja bila kupinda.
Huna haja ya kusoma kitabu chochote kupata maelezo ya kwenda huko wala hakuna haja ya kusikiliza mahubiri. Hakuna utalaamu unaohitajika , maana utajikuta umefika. Utakapofika utamkuta amekaa peke yake akiwatazama wale wengine . Hao wengine utawatambua maana ni ndugu zako wote.
Wengi kati yao ndio wale waliokuwa askari wa mwanga. Wale ambao hutaweza kuwatambua atakutambulisha kwao, na wewe utachukua nafasi yako. Usistuke utakaposikia majina yao; maana, wengi kati yao wana majina makubwa. Utawakuta wanafanya jambo fulani. Wewe pia fanya kama wao bila kuuliza , bila manung'uniko, na usikate tamaa. Kwa sasa hivi subiri ishara" ( E. Kezilahabi, Nagona)
Na kwa masikio yangu, nilipata kumsikia Philip Mangula akiyatamka haya mwaka 2007; " Isifike mahali CCM ikatangaza tenda za uongozi!" Ilikuwa ni kwenye Ukumbi wa Mikutano wa St. Dominic, Iringa, Septemba 10, 2007. Ni kwenye Mkutano wa CCM Mkoa wa Iringa.
Hiyo ilikuwa ni kauli nzito kutolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM. Mangula aliyatamka hayo wakati akitoa hotuba ya kushukuru wajumbe. Alishindwa nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa, na aliambulia kura 332.
Leo ndani ya CCM Mangula amepewa nafasi ya Umakamu wa Mwenyekiti wa CCM, Bara. Na majukumu makubwa mawili ya Makamu ni haya; Mosi, kumshauri Mwenyekiti, Pili, kusimamia maadili. Na tayari Mangula ametamka, kuwa ndani ya miezi sita atakuwa ameshakisafisha chama chake. Swali; Je, atawageukia pia ' waliomdhalilisha kisiasa' pale Ukumbi wa St. Dominic Iringa mwaka 2007?
Naliona tatizo linaloikabili CCM kama Chama cha siasa..... Soma zaidi... http://www.kwanzajamii.com --Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk
CORE 2 DUO
2.0 GHZ CPU
2 GB RAM
DVD/CD - RW
WINDOWS 7 /WINDOWS XP
WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0718 637905
0786 806028
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments