[wanabidii] WAZANZIBARI WASIOTAKA MUUNGANO, WANA HOJA -WAPEWE NAFASI, WASIKILIZWE

Wednesday, October 10, 2012

Ndugu zangu,
Kwa mara yangu ya kwanza kabisa, naomba nitoe maoni yangu kuhusu mstakabali wa "Muungano" wetu hasa suala la vuguvugu la wanaotaka muungano huo upitiwe upya!!
Mengi yamesemwa na watu mbalimbali, wasomi na wenye kujua chimbuko na historia ya muungano huo!
Lakini, watu wengi wamekuwa wakiwaona wale wanaopinga muungano kama watu wasio na hoja au "waasi".
Juzi katika pitia pitia kwenye mtandao, niliona blog moja ya "zinduka mzanzibari". Baada ya kusoma na kusikiliza yaliyokuwa yanafundishwa, nikagundua kuwa ipo haja ya watu hawa kupewa nafasi ya wazi ili watoe mawazo yao na mstakabali wa nchi yao!
Mimi siamini kuwa kuendelea kulazimisha watu kuishi kwenye muungano ambao hawana imani nao, ni kazi bure na italeta chuki kati ya pande zetu za muungano!!
Kimsingi,kwasasa Muungano huu unatakiwa upitiwe upya au ufe kabisa ili Zanzibar wawe majirani wema kama ilivyo Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, nk.
Kwasababu, wananchi wa kawaida, hawautaki, sasa muungano ni kwa ajili ya nani?
 

 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments