Wadau naomba kutoa Tahadhari kwa hili,na pia kama kuna mhusika atusaidie.
Jana niliamua kutumia usafiri wa treni kwenda nyumbani jioni.Nikiwa Pale Kamata mida ya saa Moja hivi.Treni ilifika na abiria tulikua weengi saaana.Iliposimama kama kawaida abiria wa Bongo tusivyokua na ustaarabu,wakaanza kugombania kuingia kwenye Treni.Wengine wakitaka hata kuingia kwenye behewa la wanafunzi wakati sio wanafunzi.Ilikua ni patashikanguo kuchanika.
Sasa
Kibaya zaidi nilichokiona na naomba wahusika watusaidie kabla halijaleta maafa ni,abiria kuanza kukimbiza treni na kudandia wakati linaanza kuondoka,huku wafanyakazi wa treni wakiwasukuma na kuwazuia wasiingie.Hii ni hatari saana Jamani na nilisikitika saana nikasema nitashare na wadau tuone tunafanyaje maana ndio usafiri wetu huu wakutupunguzia adha ya kukaa kwenye foleni muda mrefu.
Vinginevyo nitoe pongezi za dhati kwa Wizara husika na DR Harison Mwakyembe kwa juhudi za dhati kabisa alizozionyesha na kuzitekeleza.Najua hata Roma haikujengwa kwa siku moja.
Nawakilisha!!!
Jonas Kiwia | Director
Speedy Computers
Tel:+255 754882825 | Cell: +255 715882825 |
P.O.Box: 55133 | Dar esSalaam | Tanzania
Email:jonaskiwia39@gmail.com URL:www.speedycomputersonline.com
P.O.Box: 55133 | Dar esSalaam | Tanzania
Email:jonaskiwia39@gmail.com URL:www.speedycomputersonline.com
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments