KIONGOZI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka, amepanga kumwaga taarifa nyeti kuhusu kutekwa na kuteswa kwake na kisha kutupwa katika Msitu wa Mabwepande, Bunju, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa ndugu na rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka, ameliambia Mwananchi kuwa, kiongozi huyo wa jumuiya, amepanga kuanika hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari. Alisema Dk Ulimboka, atatumia mkutano huo kueleza siri ya kutekwa kwake.
"Siku yoyote kuanzia sasa umma, utafahamu ukweli halisi wa kilichompata kijana wetu. Niliongea naye juzi na amenithibitishia kuwa atakutana na waandishi wa habari na kueleza kila kitu katika masahiba yaliompata," alisema ndugu huyo wa Ulimboka ambaye hata hivyo, hakutaka jina lake litajwe gazetini.
http://wotepamoja.com/archives/8977#.UH5bsD4Jl3k.gmail --
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments