[wanabidii] SIMU ZA KIGANJANI MSAADA MKUBWA KUTOA RUSHWA

Sunday, October 07, 2012
Kumekuwa na malalamiko kuwa matumizi ya kutuma pesa kwa njia ya
simu za kiganjani yamekuwa ni njia bora sana na yenye manufaa
makubwa kusaidia kutoa rushwa.

Hali hii inaonekana katika madhari mbalimbali hasa katika changuzi
mbalimbali kwani simu hizo hazina tabu la msingi ni kujua namba yake
ukimaliza unamtumia bila ya maswali kama umepanga kutoa 50,000
basi hakuna tabu.

"Shekhe Makwega hapo hakuna tabu la msingi unatafutiwa namba na
kuna simu inatumika kutuma ikimaliza kazi basi chipu inatupiliwa
mbali na zingine zinahifadhiwa au kurudishwa kwa alikutuma kazi."
Kaka Kalaga bao.

La msingi ni kumjulisha tu bwana au Bi Fulani natakutimia
kiasi kadhaa kwa kulinda heshima yangu katika hili.

Sasa wadau nimepita sehemu kuna jamaa wamechukizwa na kitendo cha
kupokea bakishishi hiyo katika uchaguzi na kesho wanaelekea
huko PCCB Iringa kuweka hadharani aliyewapa mulungura na alitoa
pesa hizo kwa kusudio gani.

Lakini wanasema ngoma hiyo si ya watoto, JE ITAKESHA, MIE SIJUI
NGOJA TUNGOJE KESHO.

Wasalaam Adeladius Makwega

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Related Posts

0 Comments