[wanabidii] Sh mil. 300 Zammaliza Makongoro Nyerere, Kura Moja Ilinunuliwa Sh 300,000 hadi Sh 500,000 - Mwanzo

Wednesday, October 17, 2012

Chanzo hicho kilianika wazi kuwa, fedha hizo zilichangwa na wafanyabiashara wa Musoma, Mwanza na Arusha, ambao wapo katika mtandao wa mtu mmoja anayetajwa kuwania urais mwaka 2015.

Mbali ya matumizi ya fedha, sababu nyingine inayodaiwa kumwangusha Makongoro, ni kwamba mwaka 2010 alichangia CCM kupoteza kiti cha ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini.

Katika hoja hiyo, Makongoro anadaiwa kuponzwa na msimamo wake wa kukataa kumkana Mbunge wa Musoma Mjini Vicent Nyerere (CHADEMA), wakati wa uchaguzi mkuu 2010.

Wakati wa kampeni hizo za uchaguzi, Makongoro alitakiwa kumkana hadharani Vicent kwamba, si ndugu yake, jambo ambalo alilipinga kwa nguvu zake zote.

"Makongoro anadaiwa kuwa, mwaka 2010 hakwenda Musoma Mjini na alipotakiwa kumkana mgombea wa Chadema kwamba si ndugu yake alikataa.

"Makongoro alisema, Vicent ni mdogo wake mtoto wa baba yake mdogo mzee Kiboko, hivyo hayuko tayari kumkana ndugu, kwa sababu za kisiasa, kilisema chanzo hicho.


http://wotepamoja.com/archives/8994#.UH5kTeCS9N0.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments