[wanabidii] Mfahamu Mtanzania Aliyeuawa na Hitler - Mwanzo

Tuesday, October 16, 2012
BAYUME MOHAMED HUSSEIN, MTANZANIA MASHUHURI ALIYEUAWA NA HITLER. ALIVYOTAJIKA.

Je, ni jina jipya?, Geni au umewahi kulisikia sehemu?. Hebu leo jipe muda kumuangalia Mtanzania huyu wa tangu na Mmashuhuri wa leo katika Ukurasa huu wa "Wata nzania Mashuhuri". Hasa jina lake aliitwa Bayume Mohammed Hussein, akatajwa kuwa ni Mcheza Filamu, Askari wa Vita vile Vikuu vya Kwanza vya Dunia enzi zile za Ukoloni wa Kijerumani, wakati ambao unatajwa kuwa halali kwa Watoto kujiunga na Jeshi.

Huyu akawa Shujaa Mwenda Vitani aliyeondoka Tanzania kwenda Ujerumani ambako alifundisha na kueneza Lugha ya Kiswahili na pia aliigiza kama Askari katika Filamu anuai za Kijerumani. Katika kuonyesha namna alivyo mtafutaji asiyechoka, Bayume alifanya kazi zote ili kujipatia Mkate wake wa halali, amekuwa Mhudumu wa Mgahawa, amekuwa Baharia (mfanyakazi Melini), amekuwa Karani na kazi nyengine Lukuki tu.
Alikuwa Mtu mwema na aliyependa kusamehe hata kwa wale waliomtenda vibaya na kumdhulumu haki zake mbalimbali, dhulma na ufedhuli aliotendewa haukumpa vitisho wala kumrudisha nyuma siku zote katika kuvidai vile ambavyo ni haki kwake na anavistahili. Ni mtu mwenye Shukran kwa Mungu kwa Mitihani yote apewayo, alimtumaini Mungu wakati wote na hakukata Tamaa kwake hata wakati wa Misiba yake Mizito. "Vizuri havidumu Duniani" na "Dunia ni Uwanja wa Fujo", ndizo kauli mbili sahihi ninazoweza kuzitumia kuelezea Masikito na huzuni juu ya namna Bayume Alivyouawa kwa Uchungu zaidi katika kambi ya mateso ya Sachsenhausen kwa Amri ya Bwana Mkatili Adolf Hitler kwa sababu ya Weusi wake ambao ulionekana kama ni Uduni na Ukilema.


http://wotepamoja.com/archives/8884#.UH0uzdQ5G7U.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments