Na: Daniel Mjema, Mwanga, MWANANCHI.
WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amewataka waumini wa madhehebu yote nchini kuonyesha mshikamano katika ujenzi wa shule nchini bila kujali shule inayojengwa ni ya Wakristo au Waislam.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alitoa kauli hiyo jana wilayani Mwanga katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Kiislamu ya Lambo iliyopo kata ya Shighatini.
Lowassa alitumia fursa hiyo kusema kuwa Wilaya ya Mwanga ni ngome ya Chama cha Mapinduzi (CCM), na kwamba kwa kusema hivyo hakipigii debe chama chake bali huo ndio ukweli.
Katika tamasha la harambee hiyo iliyohudhuriwa pia na Mbunge wa Mwanga, Profesa Jumanne Maghembe, Masheikh na Wachungaji wa madhehebu mbalimbali, Lowassa alichangia Sh10 milioni.
"Mwanga ni nguzo yetu ya CCM na wala hili sio jambo la siri…Namfahamu Profesa Maghembe, katika kura hapa hamkukosea hili ni jembe…ni kiongozi hodari na mchapa kazi," alisema Lowassa.
http://wotepamoja.com/archives/9407#.UIPrXEp88ww.gmail --
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments