UTARATIBU mpya wa CCM kufanya uchaguzi wake wilayani badala ya taifani ilivyokuwa awali, umeanza kuonesha mabadiliko makubwa na athari mbaya kwa vigogo wakiwamo mawaziri.Hali hiyo imejitokeza pale ambapo baadhi ya vigogo ambao katika utaratibu wa awali wasingetarajia kuangushwa katika
kinyang'anyiro cha uongozi, wamejikuta 'wakiangukia pua'.Baada ya juzi Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kuangushwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mary Nagu, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga naye ameangushwa na mfanyabiashara maarufu Ramesh Patel katika kinyang'anyiro cha ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Kana kwamba haitoshi, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi naye ameambulia patupu katika kinyang'anyiro cha ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa. Juzi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Amos Makalla alibwagwa na Mbunge wa zamani Suleiman Saddiq Murad.http://wotepamoja.com/archives/7839#.UGpzFTqEsXE.gmail --
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments