[wanabidii] PICHA: WATOTO HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, WACHORA KATUNI PAMOJA NA NATHAN MPANGALA

Saturday, September 29, 2012

TUWAFANYE WATABASAMU


Jumamosi, 29.09.2012 Nathan Mpangala nilipata nafasi ya kutembelea watoto wanaosumbuliwa na saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuwapa zawadi na kuchora nao kama sehemu ya kuadhimisha miaka sita ya KIBONZO, kinachorushwa ITV na pia ni sehemu ya shughuli za kijamii baada ya kupata tuzo ya uchoraji bora wa katuni, 2011 niliyopewa na Baraza la Habari Tanzania.


Malengo ya ziara hiyo yalikuwa;


 (i) Kutoa msaada kwa watoto.

(ii) Kuchora katuni pamoja na watoto ili kusaidia kuwaondolea unyonge, wasiwasi, na kuwafanya kutoyaogopa mazingira ya hospitali kwani katuni zinachekesha.

(iii) Watoto watapata fursa ya kueleza hisia zao kuhusu saratani kupitia katuni hivyo kupeleka ujumbe kwa jamii kuupa ugonjwa huu uzito sawa kama upewavyo malaria, ukimwi nk.


Nawashukuru ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wa mbalimbali wa katuni walioniunga mkono katika zoezi hili. 


Pia nashukuru wachoraji katuni wenzanu walioniunga mkono kwa kuja kuchora na hawa watoto. Natoa wito kwa wachoraji katuni wengine nchini, kutenga muda angalau mara moja kwa mwaka kutembelea watoto walio mahospitalini sehemu mbalimbali nchini na kuchora nao kwani watoto wanapenda katuni.


Katuni zina mchango kiafya. Huchangamsha akili na kupunguza msongo wa mawazo. Kwa mgonjwa, tabasamu ni jambo muhimu sana.

Kama uchoraji katuni utatumika mahospitalini, utasaidia kuwasahaulisha watoto  mazingira ya hospitali kwani watajihisi kama wako nyumbani.


Mungu Ibariki Tanzania.

Nathan Mpangala

Mchoraji kibonzo - ITV

www.nathanmpangala.blogspot.com

Mobile 0713 262 902

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments