Ndugu zangu,
Jioni ya leo nikiwa katikati ya kufundisha soka ya vijana hapa Iringa nilipigiwa simu na ndugu yangu Allen, Katibu Wa CHADEMA , Iringa, akinitaarifu tukio la vurugu zilizotokea Nyololo, Mufindi na hata kifo cha Mwanahabari mwenzetu, mpiganaji Daud Mwangosi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari hapa Iringa. Kuondoka kwake kutaacha pengo kubwa. Inasikitisha sana. Ni juzi tu nilikutana na kusalimiana nae nje ya ofisi zake kwenye jengo la Mwamoto.
Pole zangu binafsi kwa familia yake ya karibu na mbali. Tuko nao katika wakati huu mgumu kwao.
Chini hapa ni baadhi ya picha nilizopata kumpiga Daud Mwangosi katika uhai wake.
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
http://mjengwablog.com
-- http://mjengwablog.com
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments