Ndugu zangu,
JULIUS Kaisari alipata kutamka; " My wife ought not even to be under suspicion"- Kwamba mke wangu hapaswi hata kutuhumiwa.
Kaisari alikuwa akijibu swali la kwa nini alimwacha mkewe Pompeia kwa tuhuma za kwenda kinyume na mienendo mema ya ndoa.
Ndio, tuhuma peke yake, hata kabla ya kuthibitishwa, zilitosha kwa Kaisari kumwacha mkewe ili alinde hadhi na heshima yake. Akiamini, kuwa wenye kuhusiana na walio katika uongozi na utumishi wa umma hawapaswi kutuhumiwa kwa kutenda yalo maovu.
Hapa kwetu haijapata kutokea, kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa kwenye tuhuma nzito ya rushwa kama ilivyo sasa. Ni vema tukatambua sasa uzito wa jambo hili; kwamba kwa Waziri mwenye dhamana kutoa hadharani tuhuma za wabunge kuhongwa ni kashfa kubwa.
Si tu kwa wabunge husika, bali kwa Bunge zima, kwa Serikali nzima, kwa nchi nzima. Hakuna dawa nyingine ya kuondokana na kashfa mbaya kama hiyo isipokuwa kwa wenye kutuhumiwa kukaa pembeni kwa maana ya kujiuzulu ili kupisha uchunguzi wa kina na ripoti yake kwa Bunge na umma.
Maana, hapa kuna mawili yanayotarajiwa kutokea pindi ripoti ya uchunguzi itakapotoka; ama kuwatia hatiani watuhumiwa au kuwasafisha na tuhuma hizo. Hilo la kwanza likitokea ni vema na busara likaendana na hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa wahusika hata kama tayari wameshajiuzulu.
Lakini, likitokea la pili, kwamba Tume iliyoundwa kuchunguza kadhia hiyo ikawaona watuhumiwa hawana hatia, hivyo kuwasafisha, basi, Waziri mwenye dhamana aliyetoa tuhuma hizo hadharani na watendaji wenzake wakuu wenye kuhusika na taarifa ya Waziri wanapaswa wajiuzulu mara moja. Ni kwa vile, watakuwa wamesema uongo.
Na hilo ndilo Neno la Leo. ( Hii ni sehemu ya makala yangu kwenye Raia Mwema juma hili)
Maggid Mjengwa,
Bagamoyo.
0788 111 765http://mjengwablog.com
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments