Salaam! Kati ya Mwaka 2005 na 2009 tulishuhudia mabadiliko ya mitaala kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya ualimu.Nilipata kuhoji juu ya mantiki ya mabadiliko hayo ya mitaala kimsingi hayakwenda sambamba na sera iliyopo ya elimu.Kutokana na hali hiyo serikali ilikuja kwa kasi ya ajabu na mjadala mpana wa sera ya elimu na mafunzo ukashika kasi.Ajabu tangu hapo sikumbuki kama uliwahi kupelekwa bungeni. Ajabu tunaambiwa tena mabadiliko makubwa ya mitaala yanakuja sijui mabadiliko hayo yataakisi sera ya elimu na mafunzo 1995 ambayo ipo au ipi? Ni mambo ya ajabu kidogo na yanatupa shida wengine wenye uelewa mdogo kuhusu maswala ya uhusiano uliopo kati ya falsafa ya elimu, sera na mitaala.Tafadhali yeyote mwenyekujua ulipoishia mswada huo atujuze hapa jukwaani.Maana pesa za walipa kodi zilitumika vilivyo kuandaa makongamano na washa kwa ajili hiyo.Tuna kila sababu ya kuhoji kuhusu mswada huo ulipofikia na sababu zilizopelekea kutopelekwa bungeni kwa karibu miaka mitatu sasa. Nawasilisha. ______________________________ A D D R E S SWithout "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity ______________________________ John J. Malata Vikindu Teachers` Training College. P.O Box 16268 DAR ES SALAAM TANZANIA Mobile: +255 754 351 868 Altenative e-mail: malata_3@live.com Blog:http://pengotz.blogspot.com/ |
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments