[wanabidii] MASHINDANO YA UANDISHI WA RIWAYA ZA KIINGEREZA KWA AJILI YA VIJANA

Thursday, August 30, 2012
Tuzo ya Burt ya Fasihi ya Kiafrika ni Mradi ulioanzishwa na Shirika la
Kimataifa la Elimu, CODE kwa ufadhili wa Bwana Bill Burts ambaye ni
Mkanada.
Madhumuni makubwa ya Mradi huu ni kuwezesha upatikanaji wa vitabu vya
kujisomea vitakavyowasaidia wanafunzi walioko katika shule za msingi
kujifunza Kiingereza ili kujiandaa kwa elimu ya sekondari ambayo
inatolewa kwa Kiingereza.
Aidha vitabu hivyo vinalenga katika kuhamasisha usomaji miongoni kwa
vijana, pamoja na kukuza uchapishaji na fasihi ya Kiafrika. Zaidi ya
hayo, Mradi unalenga katika kutambua waandishi bora wa Afrika na
vitabu bora kutoka Afrika.
Hadi sasa Mradi umeweza kuchapisha vitabu aina 9 ambavyo ni:
1. Tree land: The Land of Laughter
2. The Best is Yet to Come
3. A Hero's Magic
4. Face Under the Sea
5. Living in the Shade
6. In the Belly of Dar es Salaam
7. Close Calls
8. Lesssilie the City Maasai
9. The Choice
Miswada bora ya mzunguko wa nne ni:
1. Run Free - Richard Mabala
2. Tears From Lonely Heart - Israeli Yohana
3. Kiss Kiddo: The birthday party - Mkama Mwijarubi.
Hivi sasa miswada hiyo inachapishwa na wachapishaji waliowasilisha
miswada hii ambao ni: E& D Vision Publishing, Mkuki na Nyota na Aidan
Publishing
Mashindano ya mzunguko wa tano yataanza leo tarehe 29 Agosti, 2012
hadi Machi, 30, 2013, ambapo wachapishaji watatakiwa kuwasilisha
miswada yao katika ofisi za Mradi.
Mafaniko ya Tuzo ya Burt ya Fasihi ya Kiafrika
1. Tuzo ya Burt imeweza kuchapisha aina tisa (9) za vitabu ambazo
ni sawa na nakala 30,000. Vitabu hivi vimesambazwa katika shule 146
zilizoko katika Programu ya Usomaji, maktaba za jamii, na nakala 300
maktaba zilizoko mikoani.

2. Vitabu hivyo vimeongeza uwepo wa vitabu vya kujisomea shuleni
katika lugha ya Kiingereza.

3. Baadhi ya wachapishaji wameweza kuuza vitabu vyao katika nchi
jirani za Afrika Mashariki.

4. Tuzo hii imewezesha kutambua waandishi mahiri wa lugha ya
Kiingereza.
5. Tuzo hii inaunga mkono Mkukuta kwa kutoa mafunzo kwa wadau na
kutoa zawadi nono kwa washindi.

6. Kwa kupitia Tuzo hii waandishi wa Kitanzania wamehamasika
kuandika miswada ambayo inahaririwa na kuchapishwa kwa ubora wa hali
ya juu.

7. Warsha za waandishi zimewawezesha kujifunza mbinu za uandishi
wa riwaya kwa Kiingereza.

8. Serikali imeweza kuutambua Mradi na kumshukuru mfadhili wa
Mradi, jambo linaonyesha heshima kwa mfadhili huyo.

9. Aina 3 za vitabu chini ya Mradi vimeteuliwa kutumika kama
vitabu vya fasihi ya kiingereza kwa madarasa ya kidato cha 3-4 na 5-6
kuanzia Julai 2012. Vitabu hivyo ni Face Under the Sea, The Best is
Yet to Come na Tree Land the Land of Laughter.
Changamoto
- Wachapishaji wengi wa vitabu wako katika miji mikubwa na
hasa Dar es Salaam. Mikoani kuna wachapishaji wachache sana. Hali hii
inawafanya waandishi chipukizi kutoka mikoani kushindwa kushiriki
katika mashindano.
- Waandishi wengi hawana mafunzo ya kutosha na mbinu mbali
mbali za uandishi kuwawezesha kuandika miswada iliyo bora.
- Tuzo hii inapata ugumu wa kuwafikia waandishi wengi zaidi
hasa walio pembezoni mwa nchi.

Wito unatolewa kwa wachapishaji walioko mikoani kutafuta waandishi
chipukizi na kuwasaidia ili waweze kushiriki.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments