[wanabidii] URUSI ILIKUSUDIA NINI KUMSAIDIA TRUMP KWENDA MADARAKANI?

Thursday, August 17, 2017
Haikuingia akilini mwa wengine iliposemwa Urusi inaingilia uchaguzi wa Marekani mwaka 2016. Nakumbuka kuandika katika Facebook kuwa "Kama Trump akishinda uchaguzi, (japo nadhani hawezi) nitampongeza Putin". Baadaye Trump alishinda na ushindi wake ulionekana pale FBI ilipopotoshwa na kutangaza kumchunguza Clinton.
Inashangaza kuwa ilichukua muda mrefu kwa taasisi za marekani kugundua kuwa Urusi ilikuwa ikiingilia uchaguzi wa Marekani, na kuwa ilikuwa inasaidia Trump ashinde uchaguzi. Hii nayo si ishara nzuri kwa taifa kubwa.
Sasa hakuna ubishi. Urusi iliuingilia uchaguzi wa Marekani ikukusudia kusaidia Trump ashinde uchaguzi. Nina swali moja. Tukiona uendeshaji wa Trump wa nchi hii hukosi kuona uwezo mdogo wa mheshimiwa huyu kuimudu kazi yake. Kutoa tamko likataka kusahihishwa baada ya masaa ndio mwendo. Kukurupuka kutishia na kurudi nyuma kesho yake ni kawaida; na mambo mengine. Akifanikiwa kumaliza mhula mmoja au miwili mataifa mengi yatakuwa yameweza kujimudu kuishi bila marekani, jambo ambalo ili taifa hili liweze kuendelea kuwa kubwa lilihitaji dhana hiyo.
Sasa swali ni: Urusi (i) ilimsaidia Trump awe rais wa Marekani; AU (ii) ilimuweka Trump madarakani makusudi? Tujadili.
 


Elisa Muhingo
0767 187 507
 
--




Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.








Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments