[wanabidii] MARUFUKU YA MITUMBA: NI CHANGAMOTO AU FURSA:

Thursday, August 17, 2017
Wiki mbili hivi kulikuwa na makala katika kituo cha Television cha Star TV. Makala hiyo ilikuwa ni wageni wawili wakijadili makusudi ya serikali kupiga marufuku biashara ya mitumba hasa nguo na viatu. Kulikuwa na wageni wawili mmoja akiwa ni kiongozi wa machinga wa Mwanza. Yeye alikuwa na wasiwasi kuwa serikali kupiga marugufu uingizaji wa mitumba ifikapo 2019 inaweza kuwafanya vijana wote wanaofanya kazi hiyo ya kuuza mitumba kukosa kazi. Msimamizi wa kipindi aliweka clip ndogo ya waziri wa viwanda na biashara ndugu Charkles Mwijage kufafanua kuwa kupiga biashara ya mitumba marufuku si lengo la serikali kuwafanya watanzania watembee uchi, hapana. Anatarajia watanzania kuanza kutumia nguo zetu wenyewe kutokana na msukumo wa kulima na kutumia pamba yetu kuzalisha nguo. Bado kijana huyo baada ya clip hiyo aliona serikali inabidi kufanya kila liwezekanalo kuwasaidia wauza mitumba kufanya kazi nyingine.
 
Sikupenda kumjadili kijana huyo kwa kutoziona fursa katika mpango wa serikali, bali anatarajia serikali iwaambie la kufanya siku itakayopiga marufuku mitumba.
 
Niliamua kufanya utafiti wa kienyeji tu kwa kuwauliza watu. Kwa kuwa nilikuwa Dar Es salaam na Mbeya nimeuliza wananchi wachache wa miji hiyo. Kwa ufupi asilimia mia ya wale niliouliza wanaamini kati ya wananchi 10 wa Tanzania, 8-9 wanavaa mitumba. Nilianza kujadiliana nao juu ya fursa hii kuelekea Tanzania isiyo na mitumba. Hii ina maana kati ya watu kumi ni wawili tu ndio wanashughulikiwa na wafundi vyerahani tunaowaona wamezagaa mijini na vijijini Tanzania.
 
Hii inaonyesha kuwa twaweza kufundisha mafundi vyerahani mara nane zaidi ili kukidhi mahitaji ya uvaaji Tanzania bila kufikiri nchi jirani ambazo hatakama hazijapiga marufuku nguo za mitumba lakini tukiweza kushindana na mitumba sawa.
 
Nikaongea na baadhi ya mafundi vyerahani wanavyoweza kuundaa vikundi na kushona pamoja. Lakini wakawa wanachukua nguo ya mtumba inayopendwa sana na kuanza kuifumua na kuishona. Wakifanya hivyo mara kadhaa watakuta wamejenga uzoefu wa kushona nguo hizo zinazopendwa na watu kutoka mitumba. Baada ya hapo wamuombe mtaalamu wa mahesabu awaambie garama za kuzalisha nguo hizo na walinganishe na zile za mitumba. Kumbe wakifika hapo ni kuiambia serikali tofutti ya bei na kama za mitumba zina bei ya chini waiombe serikali ipunguze kodi mahala ili nguo za mitumba zishindane na za nchini. Baada ya hapo serikali ikipiga marufuku uwezo wa wananchi kumudu nguo za nchini utakuwa ule ule. Na kwa sababu wazalishaji watakuwa na kazi hiyo, machinga badala ya kununua mabelo ya mitumba watanunua kwa wazalishaji wa kitanzania.
 
Lakini kitendo cha kiongozi wa machinga kutoona fursa katika kusudi ya serikali twaweza kusema ni kiwango cha elimu inayotolewa katika shule zetu kuanzia ya msingi mpaka sekondari sasa.
 
Rwanda ni nchi mojawapo inayokusudia kuzuia uingizaji wa mitumba ifikapo 2019. Nimesikiliza kwa ufupi program Fulani katika Rwanda TV. (Watanzania Fulani wanaona fahari kutosikiliza TV yao yaani TBC. Hili tutalijadili siku nyingine). Katika TV ya Rwanda nimemsikia kijana akiongea kwa ufasaha katika lugha ya Kinyarwanda. Anasema: Ukienda ulaya utakuta clubs. Kuna club ya mabinti mabikra. Wana T Shirts zao wamevaa. Zimeandikwa: "trust me; I am virgin" yaani "Niamini; mimi ni bikra". Akasema wakizichoka T shirts zao wanazileta huku kama mitumba. Unakuta mama fulani mwenye mimba ya myezi sita anatembea mjini na mume wake na mtoto wao wa myaka mitano amevalia T-shirt hiyo.
Japo sikuendelea sana kusikiliza TV hiyo lakini kwa kiasi nilichomsoma Kagame, nikajua huo ni mkakati wa kuwasaidia wanyarwanda kuielewa serikali yao.
 
Natamani na vijana wa Kitanzania wangemuelewa Mwijage. Wakimuelewa; marufuku ya mitumba kwao itakuwa fursa. Sio changamoto. Tutaviona vikundi vya mafundi vyerahani vikiibuka na kuanza kushona nguo za kisasa. Tutaona ongezeko la mafundi viatu. Tutaona biashara ya ngozi ikiongezeka. Usishangae Mbuzi wale wa Iringa nao wakawa hawatupwi na ngozi zao. Kazi itakuwa kuingiza nchini majora ya vitambaa visivyotokana na Pamba. Katani yetu itazalisha vitambaa vya kutengeneza mambo mengi tu. Kumbe ni kuwaelewa viongozi wetu, kama nilivyoona vijana wa Rwanda wakisaidiana kuelezana sera za nchi yao.
Tuwemo. Tanzania ya viwanda ni kupitia mambo madogo kama haya.
 
Elisa Muhingo
0767 187 507
 


--




Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.










Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments