Nilichosema ni kuwa Tanzania imewakamata watengeneza magobole ambayo (magobole) yalikuwa hayakutengenezwa kwa kibali. Na India hivyohivyo. Sisi watengenezaji hao wa magobole tukawashtaki kwa kutengeneza magobole hayo bila kibali cha serikali. India wa kwao ikawatafutia nyenzo wakaendelea kutengeneza magobole na (India) kuanza kuyauza nje. Sisi kwa kuwa tulikuwa tunatafuta bunduki za kulinda magereza yetu tukagundua kuwa zile zinazouzwa India zinatufaa. Tukazinunua na zikasaidia maaskari magereza wetu kulinda wafungwa wetu wakiwemo wabunifu wetu wa magobole. Nilipokuwa naandika makala hiyo kulikuwa na kesi mahakamani na watu hao walihukumiwa vifungo kweli. Siyo India peke yake inayogeuza 'uhalifu' kuwa Fursa. Uganda enzi za Obote ilikuwa na shida ya waganda kutengeneza gongo wakati gongo hilo ni haramu. Baadaye uongozi wa Obote ukachemsha kichwa (okufumba omutwe). Wakawageuza wapika gongo kuwa wakala wa 'Uganda Waragi'. (kwetu ni Konyagi) hivyo Uganda waragi ikawa inanunua Gongo na kulichuja na kuliweka kwenye chupa hivyo tatizo likapungua, (halikuisha).
Tanzania ina dira yake sasa. Tunataka kujenga uchumi wa kati ifikapo 2025. Njia moja wapo ni kukuza viwanda. Huo ni mpango wa Taifa. Si serikali peke yake inayotekeleza pango huo. La! Serikali, Taasisi za kidini, Wananchi, wataalamu wa kila sekta, wanasiasa-wote tunatekeleza hilo. Ndiyo maana wanaoona; vyama vya siasa walipofungiwa kufanya mikutano ya kikampeni-tuliunga mkono. Tunaona wanataka kutupotezea muda kwa kisingizio cha demokrasia.
Moja kati ya mikakati ya kutekeleza lengo hilo la taifa wakajitokeza watanzania wenzetu wasomi wa mambo ya afya katika ngazi ya kati (Matabibu) wakafanya utafiti kwa kuoanisha magonjwa wanayoyajua kitabibu; na matibabu ya kienyeji (Kiasili). Serikali kwa kutambua hilo ikawawekea utaratibu. Waitwe watoa tiba ya asili au tiba mbadala.
Dawa ya kutibu malaria (kwa mfano) kwa dawa ya kienyeji, ni bakuli moja ya lita moja mara mbili kwa siku. Wao kwa kuangalia ukubwa wa lita na uwezo wa kuitumia wakajitahidi wakaiweka katika unga na sasa wamefikia hatua ya kutumia unga wa kijiko kimoja kwenye glass ya maji. Ni hatua hiyo.
Watu hawa wameendelea na sasa wana clinics nyingi na zinatibu magonjwa ambayo baadhi yameshindikana katika hospitali zinazoitwa za kisasa.
Dawa zao zimepiga hatua kutoka kibakuli cha lita moja mpaka glass moja. Wamepiga hatua kiasi cha kutengeneza vifungashio vizuri tu vya kisasa. Wakasema sasa huduma zao ni za 'kisasa'. Kwa neno hilo wakafungiwa.
Majuzi rais wetu amewakaribisha wahindi kuja kuwekeza katika viwanda vya madawa, badala ya kuendelea kutuuzia dawa. Ukienda India baadhi ya viwanda vinavyotuuzia madawa hayo viko uwani mwa nyumba za kuishi. Wanachofanya ni kutumia majina ya viwanda vikubwa na luweka 'label' zao na kuwalipa kamisheni. Ndizo tunazotumia na huwezi kujua labda Mwijage (waziri wa viwanda) akienda huko. (Namuamini ana uwezo wa kugundua hilo. Wengine hamna).
Miti inayotumika kutengeneza dawa ya Malaria ni Cinchona na imezagaa na ndiyo Bukoba wanatengeneza dawa za 'Omushana' lakini China wanatuletea Malaraquine. Dawa za Dr Mwaka tunasema za asili na akisema za kisasa tunamfungia lakini za Mchina tunazikubali na kuziita za kisasa. Tofauti ya dawa hizi ni moja: za wachina hatujui wanakozitengenezea. Ndiyo tofauti. Kumbe akina 'Dr. Mwaka' wa China walisaidiwa na serikali yao na sasa wanatuuzia dawa na sisi tumefaulu kuwanyamazisha wabunifu wetu sasa tunataka 'Dr. Mwaka' wa kichina na wetu tunaua. Dr. Mwaka akikosea akaenda china na kuanzisha kiwanda akaiita 'hwa ngwi chi', dawa zake zitanunuliwa tena kwa garama kubwa na kutumika katika hospitali zetu za kisasa.
Hivi muda tunaotumia kumlaumu Dr. Mwaka na wenzake kwa kutumia neno 'matibabu ya kisasa' badala ya 'asili/mbadala' kwa nini tusiutumie kumsaidia kuzifanya dawa zake za kisasa? Kama tumehakikisha zinatibu; kama tumehakikisha zinaboreshwa kutoka bulkiness mpaka small packages; Kama amefikia hatua ya kuzifungasha vizuri-tunashindwa nini kumpeleka mbele akawa wa kiwango cha kisasa?
Kwa kuzima ubunifu Tanzania inaweza kusifika. Ukiondoa swala la magobole, tunakumbuka jinsi Mafuta ya Ubuyu ulivyozimwa. Ukienda Dodoma vijijini kukutana na mzee wa myaka 120 anakimbizana na mbuzi kama kijana ni jambo la kawaida. 'Watafiti' wa kyenyeji/asili/mbadala wa kitanzania wakahusishaa matumizi ya mbegu za ubuyu na uzee mwema huo. Wakafanya utafiti; wakayakamua na yakaanza kuwasaidia watanzania kiafya na kiuchumi. Akakurupuka huko mtu na kusema mafuta hayo ni 'hatari kwa binadamu'. Kulikuwa na uvumi kuwa kuna mtu mmoja alitaka kuhodhi soko la mafuta hayo na akaanza kwa kuzima wanaoyauza. Kwamba ni kweli au sio hiyo siri kubwa.
Sipendi kuamini kuwa katika amri hii ya matibabu kufungiwa ina swala la mahusiano ya mtu na mtu kwa makusudi ya kukomoana. Tunafahamu kuwa kuliwahi kutokea mzozo kati ya uongozi mpya wa wizara ya Afya na Clinic ya Dr. Mwaka. Lakini nadhani hakuna mahusiano na si kusudi la makala hii kulijadili. Kalamu imeteleza tu.
Ninachosema ni kuwa Tanzania inahitaji kufanya zaidi ili kukuza sayansi. Lazima tujipe nafasi ya kutumia akili zetu.
Nimesikia habari za uanzishwaji wa ''Jiji la sayansi'. Nilisikiliza sana nikahofu tunaanza jiji hilo na kosa la msingi ambalo litatupoteza njia. Mpango wa jiji hilo ni kuwa Mtu mwenye degree akiwa na wazo la ubunifu atapeleka wazo hilo. Wataalamu wenzake watalipitia na lifanyiwe kazi. Najiuliza Wasomi wetu wenye degree wamewahi kubuni nini kinachosaidia jamii. Waliofungiwa wote wako ngazi ya kati. Matabibu; yaani Clinical officers (au Clinical Assistants). Kama tutajikita kuwatumia wenye degree tu basi kukwama kwa kutimiza lengo la kuanzisha jiji hilo kutaanzia hapo.
Elisa Muhingo
0767 187 507
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments