[wanabidii] MATAMSHI YA LISU: MADAKTARI WA MILEMBE WALITOA KWA LUSINDE SIRI ZA MGONJWA?

Thursday, June 30, 2016
Baada ya matamshi tata fulani ya Tundu Lissu Mbunge wa Mtera Lusinde alitoa matamshi mengine ambayo wengi tuliyachukulia kama mizaa ya kisiasa. Lusinde alisema Tundu Lisu ana file Milembe. Milembe ni hospitali maalum kwa wagonjwa walio na matatizo katika mifumo yao ya akili. Kwa kawaida watqnzania wanaichukulia kama hospitali ya vichaa. Kitaalamu sio lazima mtu awe kichaa ndiyo ahudumiwe Milembe lakini vichaa na matatizo mengine ya mifumo ya akili.
Moja kati ya njia za kutambua matatizo katika mifumo ya akili ni matamshi. Sio mpaka kuvua nguo. Matamshi yaliyopitiliza au yasiyoendana na mazingira ni dalili za matatizo katika mifumo ya akili.

Kuanzia Bunge Maalaum la Katiba Tundu lisu amekuwa akitoa matamshi yanayopitiliza. Mfano hai ni Matamshi ya Lisu kuhusu Baba wa Taifa. Matamshi yake hayakutosha kufikiri kuwa Lisu ana file Milembe ndiyo maana Lusinde aliposema Lisu ni mgonjwa wa akili wengi tulimpinga na kusema ametia chumvi katika kumtathmini Lisu. Kuanzia hapo ufuatiliaji umekuwepo na kwa kweli matamshi ya Lisu kuhusu kiongozi wa Taifa (Rais) majuzi, yamedhihurisha pasipo mashaka kuwa mfumo wa ubongo wa Tundu Lisu unaweza kuwa na matatizo, kwa hiyo si ajabu kukuta ana file katika Hospitali ya taifa ya wagonjwa wa akili. Hoja na haja yangu ndogo ni kujadili kama Madaktari wa Hospitali ya Milembe wametoa siri za mgonjwa kwa Lusinde? Nini implication yake kwa kuzingatia kuwa mgonjwa mwenyewe ni mwanasheria nguli nchini?
Elisa Muhingo

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments