[wanabidii] WAINGEREZA NA WAMAREKANI KUVUTIWA NA UTENDANI WA MAGUFULI: LAZIMA KWENDA NAO KWA TAHADHARI.

Sunday, May 15, 2016
Nilitaka kujiuliza kwa nini Rais Magufuli hakwenda kushiriki mwaliko maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza D\vid Cammeron, kujadili rushwa. Badala yake akaamua kuwakilishwa na Waziri Mkuu wake na yeye kwenda kushiriki kuapishwa Rais Museveni wa Uganda.
Ilipotajwa kuwa ni kwa sababu ya Uganda kuipatia Tanzania nafasi ya bomba la mafuta kupitia Tanzania nilitaka kushawishika.
Baada ya kusoma habari za Uingereza na Marekani kuvutiwa na 'utendaji' wa Magufuli nilianza kuhisi kuwa Magufuli si kwamba hakwenda bali 'alikwepa' (au alikacha) kwenda huko.
Ninaamini mabwanyenye hawa wanamsoma Magufuli na yeye kawahisi naye kaamua kuwasoma kwanza pia.
Rais mstaafu Benjamin Mkapa alipoingia Madarakani alilenga kulikomboa taifa hili na Mwalimu Nyerere alimtegemea. Aliondoka madarakani akiwa amelipa madeni na Tanzania ikawa katika mazingira mazuri ya kukopesheka na hivyo kuwa na msingi mzuri wa kuendelea. Nani alimsaidia Mkapa 'kubinafsisha' kila kitu ikiwemo na benki ya wanyonge (NMB) ni vigumu kujua.
Mwaka 2005 wakati JK akiendesha kampeni za kugombea urais Waziri wa mambo ya nchi za nje 'mwenzake' wa Marekani alizua mkutano unaosemekana haukuwa na agenda (maalum au ya maana). Akamlazimisha Kikwete kuacha kampeni kwenda kushiriki mkutano huo. Kikwete inasemekana alimuuliza Rice kwa nini amemualika hasa. Condoresa Rice alijibu kuwa alitaka kumuona kwa mara ya mwisho akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania, (haya yaliandikwa kwenye gazeti hapa nchini). Kikwete alipoingia madarakani kwanza alikwepa uenyekiti wa AU kama sio wa Commonwealth (sikumbuki vizuri). Alipoulizwa kwa nini alisema ana agenda na vipaumbele vyake. Tunaona mwisho wake ambao hata kama kuna udhaifu wake binafsi, lakini mabwanyenye hawa lazima waliutumia. Sina hakikia Kiwango cha madeni alicholipa Mkapa (yaliyotengenezwa toka awamu ya kwanza nay a pili) na haya aliyoyaacha JK (yaliyotengenezwa katika myaka yake kumi) kipi ni kikubwa. Tulikopa kufanya nini, sijui pia. Lakini hii misaada ya 'Capacity Building' inayowaweka watendaji wa hospitali zetu kwenye semina zisizoisha ni mojawapo. Ninaamini misaada hii itatuumiza kuliko kutusaidia licha ya kuwa inatatua 'matatizo' ambayo hatukuyaona sisi bali 'wanaotusaidia'.
Magufuli kaingia kwa gia inayoelekea kulibadili taifa hili. Wenye akili tunajua mataifa haya makubwa hawapendi kuona nchi inainukia kiuchumi ndiyo maana wanataka kuhakikisha wanakusaidia kwendelea ili ukomee wanapoona na wanapotaka. Ukibisha watamtafuta 'Savimbi' nchini mwako watamuweka ataku'Angola tu. Au watampata 'Mobutu'. Ukishindikana watakubatiza kama alivyobatizwa Ghadafi na kuitwa Muuaji na dictator. Au 'utakutwa' na silaha za maangamizi kama Husein (Sadam).
Ukitaka kujua Mkutano huu wa Cameron umezuka lini na una maana gani; uanzie pale Marekani walipomuona Magufuli kiongozi mbaya na kumnyima misaada kupitia MCC lakini ndani ya kipindi kifupi sasa kiongozi huyo ambaye hajabadilika wala kubadili mfumo walioulaumu kawafurahisha wamarekani na wanaanza kumsifu na kuamua kulisaidia taifa lake. Mtu akisema mkutano uliandaliwa mahsusi kwa ajili ya kumpata Magufuli siwezi kubisha japo alikuwa 'Mwalikwa tu' kutoka Africa na mwenzake Buhari wa Nigeria.
Jamaa hawa wana mbinu nyingi. Siwezi kushangaa kama ninalolisema likipingwa au 'kutoeleweka'. Akili nyingi za watu zimetekwa. Unapomuona Muha kakulia buha toka kuzaliwa hadi kumaliza shule. Kaanza kucheza ngoma leo na kupata nafasi ya kwenda Marekani myezi sita. Anarudi lafudhi imebadilika, ujue jinsi jamaa zetu hawa walivyo na uwezo wa kubadilisha akili zetu zikubaliane na mambo yao. Kuhisi kuwa Magufuli anaweza kuwawia ngangali, tutarajie semina zaidi ambazo ataendelea kualikwa. Akishindikana watawageukia wasaidizi wake kama walivyomfanya Nyerere. Tuna kazi. Tena kubwa kufikia kushikamana na kuwaendea kijasili.
Elisa Muhingo
elisamuhingo@yahoo.com


--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments