[Mabadiliko] NIULIZE KITU CHOCHOTE KUHUSU MAKINI SMS

Friday, May 13, 2016

*
Pata elimu kiganjani mwako BURE kwa kujiunga na huduma ya MAKINI SMS na ujisomee masomo ya O-level kwa njia ya simu. Baada ya serikali kubaini kwamba wanafunzi wengi hufeli mitihani yao kwa kukosa vifaa vya kujifunzia, wadau wa elimu https://www.shuledirect.co.tz/ wakaja na wazo la kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa njia ya simu. Wanafunzi ambao tayari wamejiunga na MAKINI SMS wamefanikiwa kuboresha viwango vyao vya ufaulu katika masomo yaliyokuwa yakiwasumbua hapo awali. Hata wewe huchachelewa bado. Jiunge na uanze kusoma sasa.
 
*
BAADHI YA MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA
*
1. MAKIN ISMS ni nini?
MAKINI SMS ni huduma ya elimu inayotolewa kwa wanafunzi wa kitanzania kupitia simu za mkononi.
*
2. Huduma ya MAKINI SMS hutolewa na mitandao ipi ya simu?
Kwa kuanzia, MAKINI SMS inapatikana kupitia mtando wa tiGO pekee. Baadaye itasambaa hadi mitandao mingine ya simu.
*
3. Kama mwanafunzi hana laini ya tiGO atajifunzaje?
Kama mwanafunzi hana laini ya tiGO anaweza kununua na kuitumia kwa ajili ya kusomea huku akiendelea kutumia laini ya mtandao mwingine anayoimiliki. Hata hivyo, siku hizi mchina ameturahisishia mambo kwa kutengeneza simu zinazoweza kuingia laini nyingi.
*
4.  Mwanafunzi hujiungaje?
Mwanafunzi au mtu yeyote anayependa kujiunga na huduma hii atatuma neno MAKINI kwenda namba 15397 na kisha atatumiwa meseji atakazokuwa akizijibu (REPLY) kwa ajili ya kujisajili. Usajili unahusu jina la mwanafunzi, jinsia, shule anayosoma na kidato anachosoma. Kwa wale wanafunzi wa QT na wengine wasiokuwa katika mfumo rasmi wa shule pia wanaweza kujiunga kwa kufuata maelekezo yanayotumwa hatua kwa hatua.
*
5. Baada ya kujisajili inakuwaje?
Baada ya kujisajili utakuwa unatuma neno MAKINI kwenda namba 15397 kila unapohitaji ku-rivise topic yoyote. Baada ya kutuma hiyo SMS utakuwa unaletewa mpangilio (MENU) utakaokuwezesha kuchagua somo (Pick Subject) kwa ajili yaku-rivise na kujibu maswali, kumuuliza mwalimu (Ticha Kidevu) swali katika somo lolote (Ask Ticha Kidevu ), kutafuta maarifa au jambo lolote kwa kutumia Wikipedia, kupata matokeo ya maswali uliyojibu (Get Reports), na kuhama kidato (Change Class).
*
6. Prelude to inauguration
Kusikiliza maandalizi ya uzinduzi wa huduma ya makini SMS ambayo hatimaye ilizinduliwa manamo mnamo tarehe 18.03.2016 msikilize http://millardayo.com/gud116/ Mkurugenzi Mtendaji (MD) wa https://www.shuledirect.co.tz/ akiunguruma.
*
Kwa ufupi, hivi ndivyo huduma ya kujisomea ya MAKINI SMS inavyofanya kazi. Kwa swali lolote unalotaka kufahamu kuhusu MAKINI  SMS, unakaribishwa kuuliza kwa moyo mkunjufu.
*
#HAPA KUSOMA TU!

Share this :

Related Posts

0 Comments