[wanabidii] Sababu za Msingi kwanini Bomba la mafuta Uganda lipite Bandari ya Tanga

Saturday, March 26, 2016
Hongera sana Professor Muhongo, Dr. James Mataragio na timu yako kwa kulitetea taifa na nimepenyezewa ubuyu kuwa mambo sasa safi, Bomba ni confirmed linapita Tanga.

Miongoni mwa hoja mlizozijenga kwa mama Irene Muloni na msafara wake kutembelea bandari ya Tanga ya kwa nini wajenge bomba lao kupitia Tanzania na si Kenya ni hzi.

1. kina cha bandari ya Tanga kina urefu wa zaidi ya mita 40 wakati meli za mafuta zinahitaji mita 18 hivyo kuwa bandari salama zaidi kwa meli za mafuta. tofauti na Lamu ambapo kina chake ni kifupi mno, hivyo inabidi kuongeza kina kwa kuchimba zaidi.

2. Bandari la Lamu ina mawimbi makubwa mno, kutokana na kutokuwa na visiwa vya pembezoni mwake vinavyopakana nayo, upepo toka bahari za mbali unavuma moja kwa moja mpka bandarini, sio salama kwa meli ya mafuta ukilinganisha na bandari ya Tanga iliyoko katikati ya visiwa vya Pemba na Unguja hivyo haina mawimbi makubwa na kuwa salama zaidi kwa meli za mafuta ambazo huhitaji utulivu wa hali ya juu wakati wa kupakia shehena yake ya mafuta kwani huchukua siku nyingi sana kupakia mzigo na inahitaji utulivu sana.

3. Bandari ya Lamu iko mpakani na Somalia hivyo nirahisi kwa meli za mafuta kutekwa na maharamia ya kisomali wakati Tanga ipo katikati ya Zanzibar na Bara hivyo kuna doria za jeshi la Tanzania na vikosi vya Zanzibar hivyo sio rahisi kuvamiwa na maharamia.

4. Tanga tayari kuna miundombinu ya mafuta tofauti na Lamu inabidi ijengwe. Pia vifaa vya ujenzi vitashuka Tanga na kwenda site moja kwa moja ,tofauti na Kenya vifaa itabidi viteremshwe mombasa na kusombwa kwa maroli kwenda site.

5. Tanzania imetoa ofa ya kutenga bandari ya Tanga kuwa mahususi kwa mizigo ya Uganda na tayari kuna miundombinu ya reli na barabara ambapo Lamu hakuna reli wala barabara ya kwenda huko.

Maelezo haya yaliwaridhisha na Irene Musoni na team yake wameahidi kutuma wataalamu baada ya wiki mbili kukagua njia zitakazotumiwa kupita bomba la mafuta.

"Nimeona taarifa ya mradi iliyowasilishwa hapa na wataalamu na pia nimepata fursa ya kutembelea Bandari ya Tanga na kimsingi nimeridhika na wiki ijayo nitatuma timu ya wataalamu ili kuja kufanya uhakiki wa njia mradi utakapojengwa na mahali ujenzi wa matangi ya kuhifadhia mafuta yatakapokuwepo ili kushauri kabla ya utekelezaji rasmi kuanza,"
alisema Muloni.

Naona katoa muda wa kwenda kumueleza Uhuru kuwa dili limebuma.

>>Much Respect kwako Mukulu anko Magu kwa "kichwa ngumu" hakuna ile mambo ya kuwa soft soft, ume prove kwa watanzania kuwa wewe ni Ngosha kweli

>>Much respect kwako Silent Killer Professor Muhongo kwa umafia kwa kimya kimya ulioufanya, umelibeba taifa.

>>Much respect kwako balozi Mahiga kwa Economic Diplomacy na Intelligence
iliyotukuka.

>>Much Repect kwako Mataragio kwa agressiveness yako kuu kwa hawa manyang'au.
NB:

Nachowaomba serikali yangu sikivu ni kuona namna ya ku-mjoin South Sudan katika bandari ya Tanga awe na ka-portion kake pale maana itamuhakikishia fursa ya kupunguza hustling anazopata kwa sasa, hasa ukizingatia Mkenya hanaga jema kwa mtu zaidi ya kuangalia maslahi yake.

Lakini pia mpige hatua mbele zaidi ya kuangalia namna ya kumuamsha Mganda katika usingizi mzito alio nao wa namna ya kuichangamkia South Sudan ili iwe partner wake kiuchumi kwa kupitisha bomba lake la mafuta Uganda kuja Tanga maana hio itamuongezea mapato Uganda pia tofauti akizubaa bomba likapitia Kenya, Uganda hatapata hata mia.

kwa hisani ya jf

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments