Unafiki na undumila kuwili kwa sasa umewaumbua. Mlificha magonjwa kwa unafiki na sasa kifo cha serikali ya umoja wa kitaifa kinawaumbua.
Mlimtumia Abubakar Khamis Bakary Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni kuwasilisha hoja binafsi kulitaka Baraza la Wawakilishi kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu kuanzishwa kwa Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar lakini katika mlengo wa kutaka kujitenga na Tanzania Bara. Hoja hiyo, ilikubaliwa na Baraza la Wawakilishi na kupelekea kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni Nam 6, 2010.
Mliamua kujifungia kwenye vyumba vya siri bila kuwashirikisha wananchi wa Tanzania Bara na mkafikia makubaliano ya kinafiki ya kubadilisha katiba yenu kwenye Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza ambayo kwa sasa inasema, Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.
Mbaya zaidi, kwa kupitia katiba yenu ya kinafiki mkatuaminisha kinafiki kuwa Tume ya Uchaguzi kwa sasa ni huru na inayojitegemea katika kutekeleza majukumu yake kupitia Kifungu cha 119 (13) kwa sababu ina wajumbe WANNE waliopendekezwa na vyama vya CUF na CCM. Mjumbe MMOJA aliyependekezwa na Rais. Jaji MMOJA aliyependekezwa na Mahakama Kuu na pia Mwenyekiti aliyeteuliwa na Rais kwa kadri anavyoona inafaa.
Mkasema wazi katika kifungu cha 119(13) kuwa: "Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba".
Hamkuishia hapo, mkatuambia kupitia Kifungu cha 119(4), kuwa pindi Mjumbe wa Tume anapoteuliwa, hakuna mtu/kiongozi mwenye mamlaka ya kumuondoa au kumfukuza Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi mpaka atakapotimiza miaka mitano tokea kuteuliwa kama Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
Tume ya Uchaguzi mkaifanya kama Jini ndani ya chupa, kwa sasa limetoka na hamuwezi kulirudisha ndani ya chupa! Mmebaki kulaumiana kuhusu nani aliyelitoa jini kwenye chupa!
Mkatuambia mmechoka kufanyiwa maamuzi na watu wa Tanganyika na kuanzia sasa vyenu ni vyenu wakati wa raha lakini wakati wa shinda, vyenu ni vyetu. Tuliwaambia haiwezekani vyenu viwe ni vyenu pekee wakati wa raha lakini wakati wa shida, vyenu viwe vyetu.
Mkasema Watanzania Bara wanachochea mtengane lakini kwa sasa mmeamua kushikamana. Tuliwaambia hiyo ndoa yenu haitadumu lakini mkabisha. Yamefika wapi?
Unafiki na undumila kuwili kwa sasa unawatafuna!
Maji mliyavulia nguo mkiwa mmejifungia ndani ya chumba cha siri, hamna budi vile vile kuyaoga.

0 Comments