1. Majaliwa ahimiza ujenzi wa miundombinu
Hii ni habari inayopewa nafasi ya kwanza kwa mujibu wa mtandao wa Mjengwablog.com. Inahusu uchumi wa nchi. Ujenzi wa miundombinu ni muhimu katika kuharakisha ukuaji wa uchumi wa nchi. ...
Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa jana alihimiza hilo kwenye ufunguzi wa mkutano wa miradi ya ubia katika ujenzi wa miundombinu kati ya Japan na Tanzania.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Majaliwa, Tanzania ina urefu wa barabara zipatazo kilomita 87, 581. Hii ni kutokana na sera na jitihada mbalimbali zilizofanywa miaka 10 iliyopita. Mheshimiwa Majaliwa aliongeza kusema, kuwa barabara za urefu wa kilomita 17, 762 zimefikia hatua mbalimbali za ujenzi.
Imesemwa pia, na Waziri Mkuu Majaliwa, kuwa Tanzania ina mifumo miwili ya reli; Reli ya kati yenye urefu wa kilomita 2,706 na reli ya Tazara yenye urefu wa kilomita 975.
Ni dhahiri, kuwa mbali ya ujenzi wa barabara, mipango yeyote ya kuimarisha usafiri wa reli ikiwamo ujenzi mpya wa reli kwa maana ya kupanua mtandao wa reli nchini, sambamba na kuimarisha zilizopo na huduma zake, kutapelekea kuongezeka kwa kasi ya kukua kwa uchumi a nchi.
Zilizofanyika miaka kumi iliyopita ni juhudi njema, na Awamu hii ya Tano, iongezea juhudi zaidi katika eneo hilo la ujenzi na uimarishaji wa miundombinu.
2. ZEC wakutana kujadili marudio ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar
Hii ni habari inayochukua nafasi ya pili kwa ukubwa. Zanzibar inahitaji utulivu wa kisiasa ili shughuli za kiuchumi ziendelee na zilete nafuu ya maisha kwa watu wengi wa kawaida. Katika mtanziko wa kisiasa uliopo sasa, hakuna namna yeyote ya kuupata utulivu huo pasipo na kurudiwa tena kwa Uchaguzi Mkuu Zanzibar, na safari hii katika mazingira yatakayohakikisha pande zote mbili hazifanyiani rafu. Ni kwa uwepo wa uangalizi wa karibu. Wapiga kura wa Zanzibar wapo. Idadi yao inafahamika. Busara kwa sasa ni kugharamia uchaguzi wa marudio kwa manufaa ya Wazanzibar wote. Demokrasia ina gharama zake, na kamwe zisiwe ni kwa roho za wananchi kupotea kwa kushindwa kuwapa fursa ya kufanya maamuzi kwa njia ya sanduku la kura kwenye uchaguzi huru na wa haki.
3. Mkanganyiko wa Elimu Bure
Hii ni habari iliyotawala kwenye magazeti mengi. Ni habari yenye kuihusu jamii ikiwamo wazazi na wanafunzi wenyewe. Kuna haja ya mkanganyiko huu kutolewa ufafanuzi wa kina ukaeleweka. Maana, kimsingi, haiaeleweka na wengi. Kuna wazazi waliotafsiri elimu bure kuwa ni kila kitu kitabebwa na Serikali. Kwamba mzazi kazi yake ni kuhakikisha anamwamsha mwanawe asubuhi aende shule. Ijulikane mapema, ni nini wajibu wa Serikali katika mpango wa elimu bure na ni nini wajibu wa mzazi.
Soma habari nyingine za ndani ikiwamo katuni bora ya siku. Ni kwenye http://mjengwablog.com
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments