' Mabehewa Matano Ya Treni Ya Mwakyembe' Yapinduka...!
Habari hii iliripotiwa jana vyombo vya habari ikiwamo redio na tv. Kwenye ITV jana ikasemwa abiria 900 walinusurika kufa!
Kwenye magazeti leo imeandikwa pia. Mtandao wa mjengwablog.cominaiona habari hii kuwa ni ya kushangaza.
Inachanganya kusikia, kuwa mabehewa matano yameacha reli, halafu hayo hayo yamepinduka. Hivyo yameacha reli na kupinduka! Wengine wanaripoti yameacha njia! Hivyo, yameacha reli na njia na kisha kupinduka! Au yote kwa pamoja.
Habari hiyo inazidi kushangaza kwa vile yaliyoacha reli ni mabehewa lakini si kichwa cha treni. Hivyo, mabehewa kuna behewa lililokiacha kichwa, cha treni, au kichwa cha treni kimeyaacha mabehewa.
Msemaji wa Shirika la Reli, Midlaj Maez naye hakuniongezea ufahamu katika lililotokea. Maez anasema; ajali ilitokea baada ya kushusha abiria. Chanzo hakijulikani inasubiriwa kamati ya uchunguzi. Lakini, treni iliyoshusha abiria na kuanza kuondoka haiyumkini ikawa kwenye mwendo mkali.
msomaji au anayeangalia tv anataka kuona picha za mabehewa yaliyopinduka. Tulichoonyeshwa jana kwenye tv ni mabehewa yaliyoacha reli. Na wale abiria 900 walionusurika kufa hawakuonekana kusimulia walivyonusurika kufa.
Hii ni moja ya habari ya kushangaza katika siku ya leo Jumamosi, kwa mujiby wa mtandao wa mjengwablog.com.
Maggid Mjengwa,
Mhariri/Mchambuzi wa habari za mtandaoni
Mjengwablog.com/Kwanzajamii.com
0754 678 252
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at https://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye4FAegX1C_r7f9NzbuoOrtiyWCni3yOtiexxrEkhgufNg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments