[Mabadiliko] Habari Kubwa 3 Za Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com

Wednesday, January 20, 2016


1. Rushwa ni kikwazo kwa maendeleo Tanzania..

Hii ni makala ya mwandishi mkongwe Balinagwe Mwambungu. Mtandao waMjengwablog.com unaipa nafasi ya kwanza kwa uzito katika habari za leo.

Balinagwe Mwambungu anachambua tatizo la rushwa huku akiunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kupambana na rushwa na kuhakikisha Serikali inapata mapato yake yanayotokana na kodi halali.

Nyongeza katika hili ni uoza wa kimaadili. Mwandishi mahiri barani Afrika na duniani, Wole Soyinka, alipata kutamka; " A moral decay is a corruption" – kwamba uoza wa kimaadili ni rushwa pia.
Leo katika nchi hii hatushangai wala hatuhoji tunaposoma magazetini kuwa Mbunge au Waziri fulani anatoa mchango wa shilingi milioni mia tano jimboni kwake, tena kutoka mfukoni mwake. Hatujiulizi; amezipata wapi fedha zote hizi? Hatujiulizi, hivi Waziri ni wa jimbo au wa taifa? Je, milioni zikimwagwa jimboni haiwezi kuwa na maana ya 'kulinunua' jimbo na kulifanya kuwa himaya yake? Mbunge au waziri huyu kwa vyovyote vile ni mla rushwa na anachangia kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

2. Maalim Seif akutana na UKAWA kujadili Zanzibar

Hii ni habari kubwa inayopewa nafasi ya pili kwa uzito. Suala la Zanzibar linahusu mustakabali wetu kama taifa. Kwa Maalim Seif kuanza kujadiliana na UKAWA juu ya Zanzibar badala ya wajumbe wenzake wa kamati ya kutafuta muafaka kunaacha maswali mengi.

3. Dar es Salaam kupata Meya Jumamosi..

Meya wa Jiji la Dar es Salaam ni nafasi muhimu sana kitaifa. Meya wa jiji ndiye mshika funguo wa lango la jiji. Utakuwa ni mchuano mkali. Ni habari yenye kuvuta wengi na inayopewa nafasi ya tatu na mtandao wamjengwablog.com

Soma habari nyingine nyingi na katuni bora ya leo. Ni kwenyehttp://mjengwablog.com

Maggid Mjengwa
Mhariri/Mchambuzi
Habari za mtandaoni/Mjengwablog.com/Kwanzajamii.com
0754 678 252

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at https://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye6R7tQ41US-gQCs89kr3APtqsgtUPEE%3DhTyA3hGrX7Tcw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments