1. Magufuli awageukia madaktari; Mkurugenzi Ocean Road atimuliwa
Hiyo ni habari kubwa katika siku ya leo na inayoshika namba moja kwa mujibu wa mtandao wa Mjengwablog.com. Hatua ya Serikali imejibu kero ya miaka mingi ya shida wanazopata wananchi kutokana na migongano ya kimaslahi ya watendaji. Mkurugenzi Kliniki ya kansa Ocean Road kumiliki duka la madawa sio sawa kabisa. Katika hali hiyo kwanini tunashangaa kliniki kukosa dawa. Baada ya Ocean Road watendaji wengine walio katika utendaji wenye mgongano wa kimaslahi waangazwe. Wakibainika wahadhibiwe.
2. Sumaye avamia eneo la ardhi na kuanza ujenzi. Hii ni habari inayochukua namba 2 kwa uzito kwa mujibu wa mtandao wa Mjengwablog.com. Kitendo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi kwa miaka kumi kuhusishwa na masuala ya kuvamia maeneo ya ardhi , na si mara ya kwanza, kinatoa taswira ya ulafi wa kiongozi. Ni moja ya kero za wananchi, kwamba baadhi ya viongozi wanahodhi maeneo makubwa ya ardhi na wengi hawayatumii.
3. Polisi wauana. Ni habari ya tatu kwa ukubwa. Imezoeleka kusikia polisi kuua majambazi, lakini polisi kuua polisi ni habari ya kustaajabisha, kama vile mbwa kumtafuna mbwa mwenzake. Tukio hili limetokea Mwanza na limevuta hisia za wengi.
Angalia pia katuni bora ya leo na habari kubwa ya michezo kwa siku ya leo. Ni kwenye http://mjengwablog.com
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments