SENSEI RUMADHA FUNDI KUELIMISHA JAMII FAIDA NA MANUFAA YA YOGA
Yoga na Mfumo wa "Endocrine Glands"
Yoga na Mfumo wa "Endocrine Glands"
Mazoezi ya Yoga, hayawezi lingalishwa na aina nyinginezo za mazoezi ya nguvu za misuli. Mbinu za kiundani zenye maigizo ya mikao ya wanyama tofauti, na kupitia mtililiko wa kuvuta pumzi, una imarisha sana nguvu mwilini kuringanisha na mazoezi ya aina yeyote ya nguvu na misuli ambayo mwisho wa zoezi mwili unakuwa umechoka, wakati yale ya Yoga, mwili unakuwa umejenga nguvu zaidi.
Kuna dalli nyingi za kupungukiwa na usawa wa kemikali ijulikanayo kama "Hormones" ndani ya damu mwilini mwa mtu. Baadhi ya mapungufu ambayo hubainika mapema ni pamoja na:
Kuumwa kichwa
Matatizo ya ngozi, kuwashwa au kuwa na mapele madogo.
Maumivu ya viungo
Hali ya kutoweza pata usingizi.
Uchovu
Kupungua kwa hamu ya unyumba au ngono.
Wepesi wa kuwa na hasira
Ongezeko la uzito mwilini.
Kuzeeka haraka.
Mazoezi ya Yoga ya nauwezo wa kuzi sisimua sehemu hizo za "Glands" na kuziamsha kwa kuweza kufanya kazi yake ya kusawazisha na kumiliki usawa wa"Hormones" mwilini.
Mfumo mzima wa " Endocrine" ni kama ufuatavyo:
The Glands ni sehemu ya mwili kama kifuko mnamo fanyizwa maji yenye dawa yaingiayo damu au damuni na kufanya kazi nyinginezo mwilini kwa mizani na makadilio sahihi. Endapo kazi yake itakuwa imevuka au kushuka, pia huleta madhara mwilini na matokea yake ni kuwa na baadhi ya hizo tabia zilizoelezwa hapo juu awali. Kemikali inayo chakachuliwa na hizo Glands, inajulikana kama "Hormones". Hizi "Hormones" zina ushawishi mkubwa katika maisha ya mwanaadam, ikiwemo; makuzi ya mwili, kusaga na kuyeyusha chakula, nguvu za mwili, isitoshe na joto la mwili, ngono, kuhifadhi au kuweka maji mwilini. Hivyo, zifuatazo hapa ni kazi na majukumu ya kila moja ya "Gland" na madhara yake isipofanya kazi inavyostahili.
1. Pineal Gland
Hii imekaa ipo katikati ya ubongo wa mwanaadam. Inakiwango kikubwa cha kupokea damu Zaidi ya viungo vingine vyote vya "Glandular" mwilini. Kazi kubwa ya Pinea Gland ni kuchakachua hormone itwayo "Melatonin" ambayo inawajibika kuhakikisha maendeleo ya hali ya kuwa "kiume" au "kike" mwilini mwa binaadam; "Seratonin", ambayo ni "Hormone" muhimu kwa maendeleo ya akili pia.
Pia, hii "Gland", inakazi nyingine ambayo ni kuangalia madadiliko ya tabia ya mwili za kila siku kama vile mabadiliko ya jinsi unavyo lala usiku au pengine mchana.
2. Pituitary Gland: Hii imepewa jina na tasisi za sayansi ya madawa kama" Master Gland", katika ukweli wa kazi yake hii nikama mnara wa usambazao mawasiliano kwenye ubongo, sehemu ijulikanayo kama" Hypothalamus" ni kiungo ndani ya ubongo kinacho miliki mawasiliano ya mishipa ya fahamu kati ya mfumo wa "Glandular "na jinsi mwili unavyo kuwa katika hali ya huzuni, sikitiko au furaha. Hii "Gland" pia humiliki hali ya makuzi na kurekebisha joto mwili. Pungufu la au ongezeko la kazi yake, husababisha makuzi yasio kawaida na kuwa kibonge au mbilikimo.
3. Thyroid & Parathyroid Gland: imekaa shingoni, na inamiliki mabadiliko ya chakula kilicho liwa mwilini "Metabolism", na kumiliki kima cha joto mwilini"Body heat". Hali kadhalika makuzi na uchafu ndani ya mwili. Panapokuwa na kasoro ya udogo au ukubwa wa miliki hii, matokeo yake ni kukasirisha mishipa ya fahamu mwilini na kuwa hoi au kuchoka kila mara. Calcium na phosphorus zinamilikiwa na hii Gland.
4. Thymus Gland: Ipo katika ya kifua, na huwa kubwa mno utotoni na mtoto afikiapo barehe inapungua kuwa robo ya umbo lake. Hii ni silaha ya kinga za mwili kwa mashambulizi ya magonjwa ya nje ndani ya mwili. Ina miliki udumishaji ulinzi wa kupambana na magonjwa nayayo shambulia mwili.
5. Adrenal Glands: Hii ipo juu kidogo ya mafigo, kazi yake hasa ni kutoa nguvu na moto la hali ya juu na kuamua penye jambo la hatari au tukio, hisia ya mwanaadam aidha uamua kukimbia au kupigana kijasili kwa kupambana na tukio lolote.
6. Pancreas: ipo chini kidogo ya tumbo na kazi yake ni kuyeyusha kemikali ijulikanoyo kama "Enzyme". Katika utumbo mdogo, inachanganya "Insulin" hormone inayo punguza nguvu za sukari katika damu. Endapo Pancreas inashindwa kumiliki vyema utengenezaji wa Insulin mwilini, basi sukari ya damu huimalika Zaidi katika mwili na matokeo yake ni Diabetes mellitus au ugonjwa wa kisukari. Pia papo hapo, Insulin nyingi nayo sio nzuri, husababisha kutetemeka na udhaifu mwilini.
7. Gonards: Uume au uuke, na kazi yake ni kumiliki kazi ya ngono. Zina changanya Endrogen ambayo ni hormone ya jinsia ya kiume, pia Estrogen kwa wanawake. Hizi zote zinafanya kazi ya tabia ya mwili wa kike na kiume kwa jinsia zilivyo tofautiana.
Maumbile ya mwili mzima wa mwanaadam , inamilikiwa na hizo Hormones. Hapo ndipo utakuta, kupitia mazoezi ya aina ya " Yoga Asanas", mwili unaweza kumiliki na kusawazisha mzani wenye kima cha wastani katika uchanganyaji wa hizo hormones mwilini.
Mafunzo ya mazoezi ya Yoga, yanadhihirisha wazi kutokana na masomo mbalimbali ya uchunguzi toka vyuo vikuu vingi maarufu nchini Marekani na kuandikwa kwa majarida mbali mbali yenye malengo ya kuielimisha jamii kuhusu afya na maumbile kupitia mazoezi ya Yogasanas.
Imeandikwa na mwalimu wa Yoga, Rumadha Fundi kupitia majarida ya chuo alicho somea filosofia ya Yoga cha "College of Neo Humanist Studies", Gullringen, Sweden na pia Tiljala, Culcutta, West Bengal, India '87.
Sensei Rumadha Fundi , Yoga & Karate Instructor.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments