[wanabidii] Viti maalum ni Kosa la kiufundi litakaloigharimu chadema 2020

Wednesday, November 18, 2015

Katibu UVCCM Wilaya Ateuliwa Kuwa Mbunge Viti Maalum Chadema


Katika hali isiyotarajiwa na wengi, Katibu wa UVCCM wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Bi. Anna Gideria ameteuliwa na Chadema kuwa mbunge wa viti maalum.


Bi. Gideria amejiuzulu nafasi ya ukatibu na kukabidhi barua yake kwa mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Manyara, Bi. Regina Ndege baada ya kutangazwa majina ya viti maalum na jina lake kuwa katika orodha ya wabunge wa Chadema.


Akizungumzia hatua hiyo, Bi. Ndege alieleza kuwa Bi. Gideria alipoteza imani na CCM muda mfupi baada ya jina la waziri mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kukatwa katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM.


Mwenyekiti huyo alieleza kuwa Bi. Gideria alikuwa 'Team Sumaye' na aliomba likizo ya mwezi mmoja baada ya jina la waziri mkuu huyo wa zamani kukatwa.


"Baada ya Sumaye kutoswa, alipoteza imani na CCM na ilipofika wakati wa kampeni mwezi Agosti aliandika barua ya kuomba likizo na kukabidhi ofisini kwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM wilaya ya Mbulu," alisema Bi. Ndege.


Tukio hilo limewashtua wananchi wengi wa Wilaya ya Mbulu ambao walikuwa wanamuona Bi. Gideria kama kiongozi na mpambanaji wa CCM kuteuliwa kuwa mbunge wa Chadema.

 

Zipo hisia za wananchi wengi kuwa huenda alikuwa anatumiwa kuihujumu CCM wakati wa kampeni.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments