Ndugu zangu,
Daily News la May 5, 1988 liliripoti taarifa kuwa Meneja Mkuu wa ATC, Shirika La Ndege la Tanzania alifukuzwa kazi kwa matumizi mabaya ya mali za Shirika la Umma.
Miongoni mwa matumizi hayo mabaya ya mali za umma ni kuchota shilingi milioni moja na nusu za Shirika La Umma kwa ajili ya kukarabati nyumba ya Shirika la Ndege la Umma aliyokuwa akiishi bila Bodi ya Shirika kuthibitisha matumizi hayo.
Jingine alijaza mafuta kwenye Landrover yake binafsi kwa fedha za Shirika La Umma. Na kingine kibaya zaidi ni Meneja huyo kuwataka mawakala wa ATC waliokuwa Dubai na Muscat wampe shilingi milioni moja fedha za mauzo ya tiketi...!
Naam, hata sasa wenye kuchezea rasimali za umma wanapaswa waondolewe kwenye nafasi hizo, tena kama ilivyokuwa enzi hizo za akina Mzee Mwinyi, kwa kuanikwa makosa yao hadharani.
Maana leo kiongozi wa umma anakusanya tiketi na risiti hewa za mafuta ya gari na kisha kudai malipo. Ni rahisi sana kuwabaini waovu hawa na kuwatimua.
Leo tunashuhudia magari ya Serikali na mashirika ya umma yakitumika kwenye masuala binafsi hata ya kwenye starehe za usiku. Watendaji kama hao walitakiwa wotolewe mfano kwa kuondolewa kwenye nyadhifa zao kwa kukiuka maadili ya kazi.
Na wanyonge wa nchi hii wamechoshwa kubebeshwa mzigo wa gharama, nyingine zikiwa ni za udanganyifu wa watendaji. Naambiwa, mathalan, kuna jamaa alipeleka risiti za chakula cha jioni na ajabu zilikuwa risiti tatu kutoka hoteli tofauti.
Sasa inawezekana vipi mtu mmoja huyo huyo awe amekula chakula cha jioni katika hoteli tatu tofauti kwa jioni hiyo hiyo, na yote ni milo ya gharama. Atakuwa ana tumbo la namna gani?!
Maggid,
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments