Muundo wa Serikali Ndogo Kuchochea Ukuaji Wa Uchumi.
Na: Jonathan N. Mnyela
Wachumi na watunga sera wamegawanyika kuhusu swala la ukubwa au ukuaji wa serikali ikiwa unazuia au kuochochea ukuaji wa uchumi katika nchi. Hivyo dhana hii ina makundi mawili..wanao kubaliana na wanaopingana na dhana nzima, lakini leo nimeamua kujikita kwenye Dhana ya Muundo wa Serikali Ndogo inavyoweza kuchochea Ukuaji wa Uchumi. Swala hili limetokana na ukweli kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuli imejikita katika kukata matumizi yasiyo ya lazima na ambayo hayana tika katika maeneleo ya nchi na ambayo hayaendani na Hapa Kazi Tu.
Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika kuhakikisha kuwa programu mbalimbali za serikali zinaleta thamani ya fedha kwenye bidhaa za umma (public goods) kama elimu, afya, na miundombinu.
Msingi wa dhana hii na watu wanaoamini katika ufanisi wa muundo mdogo wa serikali, kuwa serikali ikiwa kubwa sana tija na ufanisi wake katika matumizi na usimamizi wa rasiliamali unapunguza kwa kiasi kikubwa. Hii ni kwa sababu rasilimali nyingi zinatolewa kutoka kwenye maeneo yanayozarisha ili kwenda kuhudumia matumizi makubwa ya serikali ambayo hayana tija.
Dhana ya Uchumi wa Matumizi ya Serikali:
Dhana hii haisemi moja kwa moja kuwa matumizi ndayi ya serikali yanaweza kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Japokuwa, wachumi wengi watakubaliana na mimi kuwa matumizi madogo na yaliyo na tija ndani ya serikali yanaweza kuwa na matokeo chanya kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
Ukitazama mchoro huu hapo chini utagundua kuwa, Ikiwa matumizi ya serikali yatakuwa ni Sifuri (0) kutakuna na maendeleo madogo sana ya kiuchumi katika nchi kwa sababu huwezi kuingia mikataba, kulinda rasilimali, au kujenga miundombinu fulani fulani inayochangia ukuaji wa uchumi. KWA MANENO MENGINE, KIASI FULANI CHA MATUMIZI KATIKA SERIKALI NI MUHIMU ILI KUSIMAMIA NA KUTIMIZA UTAWALA WA SHERIA. Mchoru huu unaonyesha kuwa huwa hakuna shughuli zozote za kiuchumi ikiwa kutakuwa hakuna serikali, lakini ikiwa shughuli za msingi za serikali zikianza kupatiwa fedha maendeleo ya kiuchumi yananza kutokea.
Faidha dhidi ya Gharama: Wachumi hukubaliana kuwa matumizi ya serikali hugeuka kuwa mzigo ikiwa matumizi ya serikali yatakuwa ni makubwa sana au ikiwa mafungu ya fedha za matumizi yakipangwa vibaya (misallocated). Katika mazingira kama hayo gharama ya kuwa na serikali kubwa inazidi faida zake…na uchumi wa nchi kuanza kudorola na kudondoka..(rejea mchoro). Kuporomoka huko kwa uchumi kunaweza kutokana na sababu zifuatazo:
1. Gharama za Kupata Fedha (Extraction Cost): Matumizi katika serikali hujihitaji fedha zake kupatikana kutoka katika vyanzo ambayo huigharimu serikali. SERIKALI HAIWEZI KUTUMIA FEDHA PASIPO KWANZA KUZITOA SEHEMU. Kila chanzo cha fedha za serikali huwa kina madhara tofauti tofauti. Mfano: Kodi – hupunguza morali ya uzalishaji, pia hukungua morali ya uchapakazi wa wafanyakazi ambao hutoa PAYE kubwa, gharama kubwa za uwekezaji, kuweka amana, na njia nyingine za uzalishaji nk. Serikali ikikopa fedha kutoka kwenye mabanki, au taasisi nyingne basi kutasababisha fedha ambazo zingekuwa zimeelekezwa kwenye uwekezaji katika sekta binafsi zinaenda serikalini ili kutumika wenye matumizi yasiyo na tija, na katika mazingira mabaya zaidi inaweza kusababisha riba kuwa kubwa. Pia mfumko wa bei unasababisha sarafu ya nchi kuanguka kwa kasi. YOTE HAYA HUSABABISHA MDORORO NA MWANGUKO WA UCHUMI KWA KIASI KIKUBWA SANA.
2. Gharama ya Kuhamishia Fedha kutoka sekta ya uzalishaji kwenda serikali (Displacement Cost): Kila shilingi ambayo serikali inatumia inaanisha kuwa shilingi moja imepungua kutoka sekta binafsi ambayo ndiyo huzalisha na kuchochea ukuaji wa uchumi. Hali hii husababisha uchumi kudorola kwa sababu badala ya kuachia nguvu za uchumi uliojengwa katika sekta binafsi, ambayo huchochea ukuaji, kazi hii inakuwa chini ya wanasiasa na watu warasimu ambao huamua kiasi gani na jinsi gani fedha zitumike.
3. Gharama za Mdororo/Kudumaa: Matumizi ya Serikali huzima ubunifu. Ushindani kusababisha fedha na utajiri kuongezeka wa watu na sekta zinazozalisha. Ukuaji wa uchumi husababishwa na ubunifu, lakini sehemu kubwa ya programu za serikali huwa ni ngumu kubadilika (inflexible).
Katika mazingira hayo, bado kuna haja ya kuendelea kuangalia ikiwa juhudi za serikali ya awamu ya Tano na mpango wake wa kupunzua matumizi ya serikali yataendana na kazi ya amendeleo ambayo watanzania wanatazamia.
Na: Jonathan N. Mnyela
Mchambuzi wa Mambo ya Siasa na Uchumi wa Mtaani
--
P. O. Box 3385
Dar es Salaam
Tanzania
Alternative email: jmnyela@yahoo.com
Blog: www.mnyela4consultation.wordpress.com
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments