"Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao". [2 Nya 7:14]
Kama watu wake mwenyewe waitwao kwa jina lake, watatubu kisawasawa, kwa kuona kosa la njia yao, na kujeuka kutoka kwenye uovu ambao wamehusika nao, Mungu aliye Hai angeleta amani, angeleta usalama, angeleta nguvu kwao. Ni yeye Mungu aliye Hai ambaye anaweza kabisa kurejesha tena amani ya nchi kama watu wataenenda katika yeye. Hiyo ni kwamba, kama watarudia kujiweka wakfu, kujiweka kwa dhati kwake, kama Mungu wao, kama muumbaji wao, na kumitumikia yeye tu. Lakini wakati wanadamu wanapochepuka kutoka kwake, wakati wanaitumikia miungu mingine mingi, wapenzi wengine, hapo wataendelea kupagawa, kuteswa na chini ya maumivu katika hayo. Yeye Mungu aliye Hai hafurahishwi kabisa wakati wale wanaodai kuwa ni watu wake wanapotoka kwake na kwenda kufanya ukahaba. Hiyo inamaanisha kwamba, wakati watakapo chagua miungu ya kipagani, njia za giza zaidi ya njia ambayo ameiweka. Sasa tunaishi katika wakati ambapo kwake wengi wamepotea, wamekwenda kwenye ukahaba, wamerudi nyuma. Katika harakati za hayo yote, wanamchukiza sana yeye. Sasa yeye Mungu aliye Hai hakuiti wewe kutoka kwake na kuzurura, kuishi katika ukiwa, kuishi katika kutengwa na yeye. Lakini amekuita wewe kutemea kikamilifu, kuja katika kweli, katika rehema aitoayo. Amekuita wewe kuendelea kujiweka wakfu, kujiweka kwake kwa dhati na kujitenga kwa ajili yake, wakati wote ukiifuata njia yake. Ni yeye Mungu aliye Hai ambaye hutoa njia ambayo ni kweli na nuru, nguvu na tumaini, na rehema kwa wale waenendao kikamilifu katika yeye. Lakini wakati watu watajitenga wenyewe na yeye, na kuwaendea miungu mingine, wapenzi wengine, hapo watalipa kwa hilo. Sasa tunaishi katika nchi, mnaishi katika wakati ambapo ukahaba upo kila mahali. Hiyo ni kwamba, katika njia za makosa dhidi yake, njia za ukiukwaji, katika njia ya kuchepuka kwenye kweli. Wanadamu katika uovu wao wanatafuta kila kitu kibaya, kichafu, na kinajisi, na baadaye kudai kuwa yote ni sawa kwake. Lakini ni wajinga waishio kwenye udanganyifu wao walio utunga, wako mbali na yeye. Sasa siku hii kwamba yeye Mungu aliye Hai hakuiti wewe kutembea mbali na yeye, kwenda katika njia za wajinga, na kadhalika kuchukuliwa nazo. Lakini amekuita wewe kunyanyuliwa katika kile akupacho wewe, ambacho ni kweli, nuru, rehema na amani aitoayo. Wakati ambapo ni yeye Mungu aliye Hai ambaye utakuwa unatafuta kumpendeza, kumtii, na kumfuata ndipo utakapo letwa katika njia yake. Kwa uhakika utapewa kweli tele, na nuru, nguvu na tumaini, na amani aitoayo. Kwamba ni yeye Mungu aliye Hai ambaye kwa hakika atakuwa anawabariki watu wajitunzao wenyewe kwa ajili yake. Hiyo ni wakati wale wanaodai kuwa wake wakitembea kwa uhakika katika wakfu kwake, ndipo kwamba ataleta amani katika nchi. Lakini wakati wale wanaodai kuwa ni wake, watanichepuka, wakienda katika njia za makahaba, wakijifanya wenyewe vitanda vya uasi, ndipo kwamba nchi itateseka kwa ajili ya hayo yote. Ni yeye Mungu aliye Hai ambaye atatamka ni nini kinachojiri kama ni kirzuri au kibaya. Hiyo iko hivi, kwa maana kwamba kama watu watatembea kwa ukamilifu katika yeye, ndipo watakapokuwa na baraka zake katika maisha yao. Lakini wakati wafanyapo ukahaba, wakati wanapochepuka, wakati wafanyapo makosa dhidi yake, ndio hao watakao lipa kwa ajili ya hilo. Sio wao pekee, bali wengine watateseka vile vile kwa sababu watu wake mwenyeye hawaku tunza upendo wao wa kwanza. Ni muhimu sana kwake, kwamba watu wake kuthibitishwa kuwa waaminifu na wa kweli katika yeye. Hiyo ni kwamba waweze kuja mbele katika kweli, katika nuru, katika rehema aliyo nayo, hata kuinuliwa katika njia yake. Sasa siku hii yeye Mungu aliye Hai hajakuita wewe kumkiuka yeye, kumtenda yeye uovu, kutoka kwake na kwenda kufanya ukahaba. Bali amekuita wewe kuwa mwaminifu, kuwa mkweli, kuwa unatafuta kumpendeza yeye katika yote ufanyayo. Wakati ambapo ni yeye ambaye unatafuta kumpendeza, kumtii, na kumfuata ndipo utakapo ongozwa na yeye. Ndipo unapopewa kweli, rehema, nguvu za jinsi alivyo, kwa maana ni yeye Mungu aliye Hai ambaye mara zote yupo kukupatia wewe hayo. Sasa siku hii uonapo mtu yeyote anayejigamba na kujitutumua, na kujivuna, kana kwamba amefanya kubwa lolote, tafakari hili. Je, anamuinua yeye, au anajiinua mwenyewe na njia zake? Sasa kwamba yeye Mungu aliye Hai hajakuita wewe kuiinua nafsi yako, wala katika namna yake yeyote ile ya hila. Bali kwamba amekuita wewe kumuinua yeye, kwa maana ni yeye unayepaswa kumpendeza. Sasa siku ya leo unapo tazama uovu, ubaya, uchafu, upatikanao nchini, ni yeye Mungu aliye Hai ambaye anaweza kuyaondoa kabisa. Hiyo ni kwamba, kama wale wanaodai kuwa wake watatubu kwa uhakika, na kumrejea yeye ndipo kwamba yeye Mungu aliye Hai, atarejesha tena haki. Kwa maana aweza kufanya kile ambacho hakiwezekani kwa wanadamu, na kwamba ni yeye Mungu aliye Hai ambaye aweza kutiisha na kuondoa majeshi ya adui. Lakini wakati wale wanaodai kuwa ni wake, watakubaliana na ajenda za adui hakuna tumaini linaloweza kupatikana. Kwa ajili hiyo siku ya leo endelea kutubu kwa ajili ya dhambi, endelea kulia kwa ajili ya haki ili irejeshwe, kwa maana kwamba anawasikia wale ambao wamesimama vizuri na yeye. Kama utalia kwa uhakika kwa ajili ya watu kutubu, ni yeye Mungu aliye Hai ambaye anaweza kuwafanya hao wawe hivyo. Vitu ambavyo wanadamu hawawezi kuvifanya, anaweza kuvifanya! Kwa ajili hiyo usiangalie mazingira, kana kwamba hayawezi kubadilishwa, lakini mwaamini yeye. Lia, lia, lia kwa ajili ya toba juu ya nchi, na yeye Mungu aliye Hai atakusikia uliapo. Kwa maana kama kweli utatafuta kutembea kwa ukamilifu, kutafuta kufanya mambo yahusuyo maisha yake, nguvu yake, rehema zake, ndipo yeye Mungu aliye Hai atakapo kusikia wewe. Lakini wakati watu watakapo fanya mioyo yao kuwa migumu, wakashupaza shingo zao na kutembea mbali na yeye, ndipo maombi yao hayatafaa. Sasa tunaishi katika wakati ambapo kiburi kimeshamiri katika kila mahali na wanaume na wanawake wamechukuliwa na hilo. Hiyo ni kwamba, wamechukuliwa katika maovu ya kiburi, nao wanalipenda sana hilo. Lakini yeye Mungu aliye Hai atamsikia yeye amliliaye kwa ajili ya rehema, kwa yule amtafutaye, na kumwamini, na kumtumaini, kwamba anaweza kabisa. Iwapo ni yeye Mungu aliye Hai utajiweka mwenyewe kwake, ni yeye Mungu aliye Hai ambaye atakupa wewe maisha yake. Lakini kama ukichagua njia ya uovu uliozidi dhidi yake, ndipo unachagua giza katika nchi. Hiyo ni kwamba, kimsingi unajipeleka mwenyewe mbali na yeye, unajitumbukiza mwenyewe katika giza, na kizazi chako kadhalika. Sasa siku hii kwamba yeye Mungu aliye Hai anadhamiria kwamba watu watembee katika nuru, waipende nuru, na walindwe kwenye nuru. Kwamba ataitoa nuru hiyo wakati watu watakapotubu na kunililia yeye. Sasa siku hii wakati yeye Mungu aliye Hai aletapo nuru, itaangaza giza na ubaya, uchafu, na asili yake ya kutisha. Lakini watu wawapo kwenye mwanga hafifu kwa sababu ya makosa yao dhidi yake, wala hawaoni utisho wa giza la uovu. Hiyo ni kwamba, kirahisi hunung'unika wenyewe, hujikwaa njiani, na hawaoni vema kabisa. Ni kwa sababu katika macho yao wana vifungo vilivyoletwa na dhambi na makosa dhidi yake. Lakini wakati watu watakapo anza kutubu, na kubadili njia zao kabisa, ndipo nuru itafunua giza na italifunika. Hawatakuwa tena na urafiki na ushirika na matendo ya giza, lakini watayachukia. Watainuka katika hasira ya haki kulifukuza giza nchini. Lakini nasema wakati watu waishipo katika vurugu, ukungu wa uovu, hawaoni vizuri kabisa. Sasa siku hii yeye Mungu aliye Hai anaita kwa ajili ya watu kumrudia yeye, kutubu njia zao ovu, kuondoa kile ambacho ni kichafu mbele ya macho yake. Anawaita wale wanaodai kuwa ni wake, kuona kosa la njia zao, na kugeuka kutoka kwenye uovu wao, ambao wameuleta kwa maovu yao dhidi yake. Sasa siku hii usishindwe wala usikate tamaa, lakini uinuliwe katika yeye. Hiyo inamaanisha kwamba, unyanyuliwe katika nguvu ya uwepo wake, furaha niitoayo, kwa wote watembeao kikamilifu katika yeye. Uwe na shukrani kwamba ni yeye ambaye unaweza kuendelea kumtazama, kumwamini, kumtumaini, kumtii kwa maana yeye ndiye njia ya uzima. Siku hii yeye Mungu aliye Hai hamwiti mtu wake awaye yote kuishi katika uchafu wa dhambi, kuishi chini ya uvuli wake. Wala hawaiti watu wake kushiriki upotofu, kana kwamba ni jambo la fadhila. Lakini kwamba amewaita watu wanke kutembea katika haki, utakatifu ambao anautaka na kuuhitaji kwa watu wake mwenyewe. Kwamba anawaita watu wake kuimarishwa, kunyanyuliwa, kuongozwa na kuelekezwa mara zote na yeye. Kwa hiyo siku hii usiharakishe kwenda katika njia ya wakosaji, usiwe na haraka kuwa na ushirika na wale ambao kweli wanaishi katika maskani ya walioangamia. Lakini badala yake uharakishe kupokea kweli yake, na nuru yake ili ukaweze kwa uhakika kuwa macho na hai katika yeye. Hiyo inamaanisha kwamba, usikate tamaa kwake kwa sababu unauona uovu, unaona giza katika nchi. Lakini katika hayo yote mlilie katika toba, ukitubu kwa ajili ya dhambi, maovu ya watu wake mwenyewe ili kwa uhakika wakaweze kuona kosa la njia yao. Nasema wakati wenye haki watakapo nililia kwa uhakika, nasema kwamba nawasikia wao wanililiapo. Lakini wakati mwenye haki atakapokata tamaa katika kukosa matumaini, na kuchukia kwa jinsi mambo yalivyo, hapo watu watageukia wapi? Nasema hawawezi kufanya lolote bali kupiga mayowe kwenye upepo kwa maana mwenye haki amepoteza matumaini katika yeye. Sasa kwamba wenye haki hawapaswi kukata tamaa katika yeye, lakini wanatakiwa kuendelea kumwamini na kutumaini katika yeye. Kama kweli wataendelea kushikilia hiyo hali yao kama wenye haki, wataendelea katika matumaini kwake, kumwamini yeye, hawataaibishwa. Lakini wakati wale waliotakiwa kushikilia tumaini lao, imani yao, ujasiri wao kwake, watarudi nyuma, watakapokaa katika njia nyingine yeyote, ndipo yeye Mungu aliye Hai hafurahishwi kabisa nao. Kwa maana hawapaswi kujiweka wenyewe kwa miungu mingine, wapenzi wengine, wala hawapaswi kujiweka wenyewe kwenye kukosa matumaini, kukata tamaa, katika mambo ya hovyo ambayo ni kikombe cha wajinga. Lakini kwamba wenye haki wanapaswa kujitunza wenyewe katika msimamo sahihi kwa kubakia katika wakfu na kujiweka kwa dhati katika kusudi lake katika yeye. Nasema kama mtu awaye yote atamtumainia, hataaibishwa kwa maana ataona kwamba nafanya mambo yasiyowezekana kwa wanadamu. Lakini wakati mtu atakapotegemea mkono wa mwanadamu, wakati atakapotumainia katika mazingira, katika hali au hata namna nchi ilivyo, atakata tamaa katika kukosa matumaini. Nasema kwamba anatafuta miungu mimgine, wapenzi wengine, na kwamba atajikuta kwenye ukiukwaji katika yeye. Kwamba watu wake wanapaswa kumjua, kumfahamu, na kutambua kuwa yeye ni Mungu mtenda miujiza, ambaye naweza kufanya yasiyowezekana na ni yeye wanapaswa kumwamini. Sasa siku hii kwamba yeye Mungu aliye Hai anadhamiria wewe uendelee kutumaini, uendelee kuamini, kuendelea kumtegemea yeye. Kwamba anadhamiria wewe kumwangalia mara zote, na kujua kuwa anaweza. Wakati iwapo kuwa ni yeye ambaye utaelekezea macho yako, ambaye utakuwa unamwamini, utaona kuwa kila wakati tena, kila mara anafanya njia. Lakini kama unaangalia duniani, katika utupu, katika kupagawa, kwenye giza, kwamba unaweza kukata tamaa katika kukosa matumaini kirahisi. Sasa siku ya leo kama utafanya kweli kama alivyokueleza, kuwa tubu hata kwa ajili ya dhambi za wale ambao walitakiwa kutubu kwa ajili ya dhambi zao wenyewe, atakusikia wewe uliapo. Kwamba ni yeye Mungu aliye Hai ambaye atasikia vilio vya waliojiweka wakfu, waliojiweka kwa dhati kwake. Kama utaona kweli kosa la njia za watu, na kumlilia yeye, ni kwamba yeye Mungu aliye Hai atakusikiliza wewe. Lakini kama ukikata tamaa kirahisi tu katika kukosa matumaini na uchungu, hayo yatakupeleka wapi wewe? Kwamba yatakupeleka katika kikombe cha waovu ambapo utakunywa huko kukata tamaa, ubatili huo, giza hilo walilopo. Siku hii tubu, lia katika toba, lia katika maombezi, na yeye Mungu aliye Hai nitakusikia wewe kama kweli umejiweka wakfu kwake. | |||
|
0 Comments