[Mabadiliko] Kwenye Jamhuri Mengine Hayawezekani, Tundu Lissu Anafahamu Pia..

Tuesday, November 17, 2015


Ndugu zangu, 

Habari hiyo kubwa yaweza kuwa ni ' burudani ya kisiasa' lakini haina uhalisia.

Kwenye Jamhuri Rais akishaapishwa ndio ameshakuwa Amiri Jeshi Mkuu.Tundu Lissu anafahamu vema tafsiri ya hilo. Yawezekana, anaona, kuwa aliyeapishwa si Rais wake, nalo haliwezekani, kama Tundu Lissu atakula kiapo kulitumikia Bunge la Jamhuri, basi, Magufuli naye ni Rais wake, kwa miaka mitano ijayo.

Maana, unaposema Jamhuri haina Rais una maana Jamhuri haina pia Amiri Jeshi Mkuu. Na kwenye Jamhuri ambapo unaweza kusimama na kusema hayo na kurudi nyumbani kwa amani na utulivu, basi, ujue Jamhuri hiyo ina Rais, na hivyo, mfumo wa kidola unaoheshimu haki za raia kujieleza kwa uhuru na hata kulindwa dhidi ya watakaochukizwa na kauli zao.

Ninavyofahamu, na Tundu Lissu anafahamu hivyo, kuwa Rais atahutubia bunge, kuna wabunge wa upinzani watakaoleta rabsha za hapa na pale, na kuna watakaotulia kumsikiliza Rais wa Awamu ya Tano anatoa mwelekeo gani kwa taifa.

Na baada ya hapo maisha ya kisiasa na kijamii yataendelea kwenye 'Jamhuri ya Magufuli'- Magufuli Republic..
Goodmorning.
Maggid.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye7ejYK%3DpdHVPR8AZ%3D3oRAzM_8braFftnbz8ugQjKni39Q%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments