Usichokijua ni kuwa sheria ya Uchaguzi inasema siku ya kupiga kura hakutakuwa na mikusanyiko ya kisiasa.Mikusanyiko yote ya kisiasa mwisho wake ni siku ya mwisho wa kampeni ambayo ni tarehe 24 octoba 2015.Ukikusanya watu wako siku hiyo wawe wana UKAWA au CCM wakajikusanya mahali ni kosa kisheria.
Pili sheria ya mikusanyiko ukitaka kukusanyika lazima utoe ripoti polisi unakusanyikia nini
Tatu kuna sheria ya ardhi.Unaposema utakusanyika hapo kwenye mita 200 hilo eneo ni mali ya baba yako au mama yako? Huyo mwenye hati miliki ya hiyo ardhi karidhia?
Kaombwa kibali au unaenda tu kumfanyia uvamizi na kujikusanya kwenye eneo lake? Polisi kwa kuliona hilo kuwa kutakuwa na uvunjaji sheria kwa watu kuvamia maeneo ya watu na kujikusanya wakasema kila mtu aende kwake asubirie kwake.Wenye nyumba au maeneo ni haki yao kuita polisi wakiona mikusanyiko kwenye maeneo yao wanayomiliki.
La kwangu sikubali mtu akusanyike nakuonya mapema usisogee wala kunikusanyikia kwangu.Ole wako hiyo futi yako upime mita 200 iwe inatua kwenye eneo langu halafu uweke makalio yako hapo utanikoma.
Hii ni kutaka kuleta vurugu na ugomvi kati ya wenye maeneo na hao watu anaotaka wakusanyike hizo mita mia mbili sababu sio kwao ni kwa watu.
Kama mijini wewe ni mkazi wa eneo husika mita mia 200 itakuwa ni nyumbani kwako labda uwe umetoka mbali sababu kituo na kituo sidhani kama kinazidi mita 200.Nenda kwenu.
0 Comments