[wanabidii] Ushindi wa CUF Mtwara hauhusiki na UKAWA, ni ushindi wetu kwa nguvu yetu

Tuesday, October 27, 2015

Ushindi wa CUF Mtwara hauhusiki na UKAWA, ni ushindi wetu kwa nguvu yetu


Ladies n Gents,

Friends n Our Enemies,

First of all nachukua nafasi hii kujipongeza na kuwapongeza wakazi wa Mtwara Mjini kwenye chimbuko la vugu vugu la gesi kwa kusema kwa sauti kubwa na kuwaonesha CCM kuwa sisi tukiamua tunaweza na hilo tumelionesha.

Mtwara ni ya Wanamtwara pekee ambao bila kujali itikadi za vyama, tuungane sasa na kuijenga Mtwara yetu.. Hakuna uadui sisi sote ni Wamakonde either uwe CUF au CCM, letu ni moja.

Hongera sana mbunge mteule Ndugu Maftah.

Pamoja na kujipongeza huko, pia nichukue fursa hii kumpongeza Ndugu John Pombe Magufuli kwani kuna kila dalili kuwa yeye ndiye Rais wetu wa awamu ya Tano.

Nachukua Fursa hii kuwapa pole na kuwazomea sana Chadema kwa ulimbukeni wao wa kusimamisha mgombea wao Mtwara Mjini Ndugu Joel Nanauka kwa makusudi kabisa, ili hali wakijua fika kuwa lile ni jimbo la CUF.

Chadema walifanya hivyo kwa makusudi ili wazigawe kura za Mtwara za cCUF kama walivyozigawa kura za Segerea kwa Mtatiro na walivyozigawa kura za CUF jimbo la Mtama na kupeleka ushindi kwa CCM.

Kwaiyo sisi tunawaambia Chadema kwamba njama hiyo sisi tuliijua na tukasambaza elimu kwa wananchi ya kwamba wamchinje Joel Nanauka ikibidi wamchinje yule fisadi Lowassa ili kufanya maamuzi yenye busara..

Ikumbukwe kusini tumeanza harakati hizi tokea enzi zile za gesi, so ushindi huu ni wa kwetu kwa nguvu yetu..

Nawapa pole Chadema na nawapa pole CCM.

Mtwara ina wenyewe na wenyewe ni sisi...

Swali kwa Chadema...

Je, kwa kuwa Lowassa anatarajiwa kuanguka kwa kishindo, mkirudi bungeni mtaendeleza porojo zenu kuwa nyinyi ni wapinga ufisadi na mafisadi?

Nahitaji majibu yenu...

Kwa hisani ya jf

Share this :

Related Posts

0 Comments