[wanabidii] UCHAGUZI KATI YA UADILIFU NA UHUNI, KATI YA UKWELI NA MANENO MANENO

Saturday, October 17, 2015

UCHAGUZI KATI YA UADILIFU NA UHUNI, KATI YA UKWELI NA MANENO MANENO.

Hawa wamenunuliwa kwa sababu hamuungi mkono mtu ambaye umaarufu wake umetokana na kuwa FISADI:
1. Dr. Wilbrod Slaa
2. Jaji Joseph Waryoba
3. Joseph Butiku
4. Humphery Pole Pole*
5. Prof. Ibrahim Harouna Lipumba


Hawa hajawanunuliwa bali wamekarimiwa tu na kuona umuhimu wa kumuunga mkono mtu ambaye wao ndiyo waliwaongoza watanzania kutoa vilio vyao kuwa ni FISADI papa.
1. Fredrick Tluwai Sumaye
2. Freeman Aikael Mbowe
3. Tundu Lissu
4. Said Kubenea
5. Godbless Lema
6. James Mbatia


Miaka 50 ya uhuru serikali haijafanya kitu hata wakati hawa wakiwa viongozi wandamizi
1. Kingunge Ngombale Mwiru- tangu awamu ya kwanza hadi ya nne.
2. Fredrick Tluwai Sumaye- Waziri Mkuu Awamu ya tatu yote
3. Edward Ngoyai Lowassa-Waziri Mkuu awamu ya nne
4. Balozi Mwapachu
5. Milton Makongoro-Waziri awamu ya nne yote
6. Lawrance Masha-Waziri awamu ya nne.


Wanaondoka CCM kwa sababu mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM haukufuata utaratibu, lakini utaratibu wa kumpata mgombea wa CHADEMA na baadaye UKAWA ulifuatwa. Tehe tehe tehe tehe.


Eti Kingunge mwenye Kadi namba 8 ya CCM ameondoka iweje wengine wabaki, ila Edward Lowassa kadi ya CHADEMA ni ya kwanza kuliko ile ya Dr. Wilbrod Slaa.


Eti ni kosa CCM kusema chagua Magufuli na siyo chagua CCM lakini hakuna tatizo kusema CHAGUA LOWASSA na siyo CHADEMA.


Eti kosa kwa CCM kuimba "CCM MBELE KWA MBELE". Hivi ule wimbo wao wa 2010 wa MAFISADI bado upo?

SIASA BWANA, NI MANENO MANENO TU. MWANASIASA AKIGUNDUA WAPIGA KURA WAKE WANAPENDA MANENO MANENO, BASI ATAWACHOTA AKILI KWA MANENO MANENO.

TUTAFAKARI KWA KINA KUELEKEA OKTOBA 25, 2015

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments