Katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa kampeni za uchaguzi, sauti yangu ingekuwa "inasikika" kwa pande zote husika ningewashauri kila upende uteue mjumbe mmoja mmoja katika wazungumzaji kwenye kampeni za urais, ubunge na udiwani ambaye kazi yake KATIKA KILA MKUTANO WA MGOMBEA itakuwa kuzungumza yafuatayo kwa wafuasi wao na watanzania wote:-
1. Kumpa mpigakura elimu jinsi ya kupiga kura BILA KUIHARIBU kura yake
2. Kila mtanzania kuachana KABISA na mawazo potofu kuwa mwenye mtizamo tofauti na wa kwake amepotoka!
3. Kuwaandaa kisaikolojia wafuasi wao kupokea matokeo wanayoyapenda na wasiyoyapenda. Waeleweshwe na kuelewa kuwa "kura yako moja pekee siyo inayoamua nani ni rais wa TZ ila zote zilizopigwa bila kuharibika. Unaweza wewe na mkeo/mumeo na mwanao/wazazi wako na mpangaji wako/mwenye nyumba wako wote mkampigia mtu mmoja awe rais lakini zisitoshe - usituletee nyodo kulazimisha unavyotaka wewe iwe lazima".
+255 784 250 704
0 Comments