Mgombea Urais wa CHADEMA, Edward Lowassa kutoshiriki mdahalo wa Oktoba 18, 2015
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimethibitisha kuwa mgombea wake Edward Lowassa hatashiriki mdahalo utakaofanyika tarehe 18 kuanzia saa 7:30 mchana na kurushwa moja kwa moja na Star Tv. Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli amethibitisha kushiriki kwenye mdahalo huo sambamba na wagombea wengine.
Midahalo kabla ya chaguzi ni maarufu sana hasa katika nchi za Ulaya na Marekani. Katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Kenya ulifanyika mdahalo wa wagombea urais na wagombea wote walihudhuria mdahalo huo amboa ulikuwa kivutio kikubwa sana kwa walioufuatilia wakati huo. Mdihalo ya aina hii huwa ni kivutio kikubwa sana kwa watazamaji hasa kutokana na maswali ya papo kwa papo na pia watazamaji huvutiwa zaidi na wagombea wanaoweza kujieleza na kuchambua hoja kwa ufasaha.
Kwenye uchaguzi wa mwaka huu, wagombea wanaochuana vikali ni Lowassa na Magufuli na watazamaji wengi walitarajia wagombea hawa wawili kushiriki katika mdahalo huo wa kihistoria. Cha kushangaza, Lowassa ameingia mitini na ameukacha mdahalo. Sababu za Lowassa kuukimbia mdahalo ni hizi hapa;
1. Afya ya Lowassa, kutokana na hali yake ya afya kuwa ni ya kusuasua, na muda utakaotumika kufanyika mdahalo husika ambao utakuwa ni zaidi ya saa nzima na nusu, mgombea huyu imeonekana hataweza kumudu kusimama wima kwa muda wote huo. Ikumbukwe kuwa hata kwenye kampeni zake mgombea huyu amekuwa akisimama kwa dakika kumi tu na sio zaidi ya hapo, tofauti kabisa na mpinzani wake ambae ameonekana kuwa ngangari kweli kiasi hata kupelekea kupiga push ups jukwaani, kitu ambacho Lowassa hawezi.
2. Uwezo mdogo wa kuchambua hoja wa Lowassa, hili pia ni tatizo kubwa na uongozi wa UKAWA walishaliona hili mapema hata kabla ya kumkaribisha Lowassa kwenye chama chao. Mtakumbuka Mbowe aliwahi kukaririwa akisema CHADEMA hawawezi kumchukua "bubu" na kumfanya mgombea wao.
Lowassa hana uwezo wa kujieleza kikamilifu na kuchambua hoja kikamilifu. Mgombea ambaye hawezi kuchambua hoja, ukimpeleka kwenye mdahalo ni kujitafutia aibu mbele ya jamii ya kimataifa hasa ikizingatiwa kuwa mdahalo huo utaonyeshwa moja kwa moja na Star Tv ambayo watu wengi sehemu mbali mbali duniani wataufuatilia online. CHADEMA wanalifahamu hili na hawako tayari kuaibika. Kwa upande wa Dk Magufuli, katika kuchambua hoja yuko vizuri sana na wengi mliomsikiliza kwenye kampeni zake mtakubaliana na mimi bila ubishi.
3. Kupoteza Kumbukumbu kwa Lowassa, hili pia ni tatizo kubwa sana la mgombea huyu wa UKAWA. Kwenye mdahalo mgombea anakuwa amesimama peke yake na kujibu hoja zinazokuwa mbele yake. Lowassa hana kumbukumbu na mara zote anahitaji mtu wa kumuweka on track. Mara nyingi amekuwa akiongea hili na baada ya dakika mbili na nusu anakuwa amesahau alichozungumza. Hilo ni janga kwa
UKAWA na wanalifahamu fika. Kwa hali tu ya kawaida mgombea huyu angechekesha umma kama angeruhusiwa na chama chake kushiriki mdahalo huu. Kwa upande wa Dk Magufuli, hapo kwenye kumbukumbu hakuna ubishi kwani yuko vizuri sana, wengi mtakuwa mashahidi kwani Dk Magufuli anauwezo wa kukumbuka hata idadi ya samaki waliokuwa ziwa victoria wakati akiwa Waziri wa uvuvi.
Kutokana na sababu hizo hapo juu, Lowassa hawezi kushiriki mdahalo huo. Hii itakuwa kete kubwa sana kwa mpinzani wake mkuu Dk Magufuli ambaye kama atashiriki mdahalo huo kama ilivyopangwa, basi baada ya mdahalo huo, ambao bila shaka utamuongezea sana umaarufu ambao tayari anao, atakuwa anasubiri tu kuapishwa kuwa rais mpya wa Tanzania mpya. CHADEMA wateleta visingizio vingi sana lakini ukweli ndio huo.
. Wengine watasema mara ooh mbona CCM hawakushiriki mdahalo wa mwaka 2010? Lakini wakae wakijua kuwa CCM ya 2010 sio CCM ya 2015. Sasa hivi CCM ni kama imezaliwa upya, hasa baada ya kumsimamisha Dk Magufuli kugombea urais na kuondoka kwa wanachama "makapi" na kujiunga na UKAWA, na kuifanya CHADEMA kuwa kama CCM B.
Watanzania tunausubiri mdahalo huu kwa hamu kubwa jumapili
0 Comments