[wanabidii] Islamic Foundation yawataka Waislam kuondoka vituoni baada ya kupiga kura

Saturday, October 17, 2015
Waislam wametakiwa kutokuwa sababu ya kutovurugika kwa amani nchi Tanzania na kutakiwa , watakiwa kukaa kwa amani kwani katika mazingira ya amani pekee ndiyo yatakayowawezesha kuweza kufanya ibada zao kwa uhuru na bila ya bugudha na usumbusu wowote huo.

Hayo yamesemwa ma mwenyekiti wa Islamic foundation Sheikh Arif Nadi, ambao pia ni wamiliki wa Redio imani, Tv iman pamoja na gazeti imani vyote hivyo vipo mjini Morogoro. Amewata waislam wasiwe chanzo cha kuvuruga amani na waangalie nchi za za kiislam ambazo hazikuwa na historia ya kutoa wakimbizi, ambazo sasa zimekuwa zikipeleka wakimbizi katika nchi za ulaya kwa sababu tu ya kukosa amani, wananchi wa nchi hizo wanaishi kwa shida na tabu kiasi ambacho wanashindwa hata kufanya ibada kwa uhuru kutokana na hali ya nchi zao kutumbukia katika vurugu ambazo zinawafanya wengine kufa baharini kutokana n kukimbia nchi zao

Sheikh Arif Nadi pia amewataka waislam wote kushiriki uchaguzi mkuu na kwa amani kwa kwenda kupiga kura kasha kurudi majumbani kwani hawawajibiki na kulinda kura hiyo ni kazi ya mawakala wa vyama vya siasa, ameongeza kuwa kukaa vituoni kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani hgali ya kuwa uislam unawataka waislam kuwa walinzi wa amani badala ya kuleta visababishi vya uvunjifu wa Imani.

Wakati huo huo mkurugenzi mkuu wa Islamic Foundation sheikh Ibrahim amewataka wagombea kuwekla ahdi zinazotekelezeka badala ya kuwaongopea wnanchi kwa ahadi ambazo hazitekelezeki hivyo kuleta mkanganyiko katika jamii.

Sheikh Twaha amesema kuwa unapowaahidi watu jambo ambalo kiuhalisi halitekelezeki ni moja ya sababu ya kuvuruga amani klwani itafikia hatua watu wataanza kuhoji ahadi ulizoahidi hivyo hali ambayo inaweza kushusha vurugu.

Chanzo Redio/tv kipindi amani

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments