Hongera Dr John Pombe Magufuli
Nami nichukue nafasi hii kumpongeza Dr. JJP Magufuli; Rais ambaye ni mwajibikaji. Nchi hii ilipo inahitaji Rais kama huyu awahimize vijana waache kukaa vijiweni wafanye kazi yoyote ambayo ni halali kwa faida yao
Ni jambo la heri kuwa hatimaye Kiu ya Watanzania imetulia. Ni aina ya kiongozi tunayemuhitaji sana hasa katika kipindi hiki ambacho walio wengi wamekata tamaa ya maisha kutokana na kupanda kwa gharama za maisha kila kukicha.
Tunaamini yote yatawezekana, mradi amtangulize Mungu mbele na sisi pia tuna jukumu kubwa la kumwombea afya nzuri ili aweze kuyatekeleza yale ambayo tunayahitaji kadri ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Sina uhakika nma mihemuko ya vijana huko kijijini kwetu lakini kwa Dar it's like watu walikuwa wameaminishwa eti ENL atakuwa anapita anadondosha neema tu. Pengine ni kutokana na na zile kauli kama ".. kila mwenye boda boda moja atapata 10. etc etc etc." nakadhalika ambazo they are next to impossible!
John Pombe Magufuli ni binadamu kama mimi na wewe na jukumu la kuijenga nchi hii linatuhusu wote kwa pamoja. Tuwajibike na tufanye kazi kwa ufanisi na mustakabali wa nchi yetu.. Kidole kimoja hakivunji chawa..Tuwajibike kwa pamoja (Responsible Citizenship)
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu ibariki serikali mpya ya awamu ya Tano, Amani, Umoja, Upendo na Mshikamano vitamalaki ili tuione nchi ya Maziwa na Asali kupitia uongozi wa Mteule - Dr John Pombe Joseph Magufuli..
Omukunirwa Ireneus
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAN5khk78kRm6W%2Bxru8zQQChzo6Wt3gWCShxUa80Jc7WXmcGTtA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments