Tanzania imeendelea. Kuna mambo mengi yamefanyika. Kuna mambo mengi hayajafanyika. Ambayo yamefanyika ni msingi wa kufanya ambayo hayajafanyika. Kwa yale ambayo hayajafanyika kuna sababu mbili 1) Hayajafanyika kwa sababu ya yale yaliyofanyika. Mfano tusingeweza kuanza kuchimba gesi kabla ya kuigundua. 2) kwa sababu ya uharibifu, uzembe nakadhalika. Ndiyo maana kuna uchaguzi. Uchaguzi ambamo tunaweza kubadilisha viongozi au hata chama. Kabla ya kufanya uchaguzi tunavichunguza vyama, hasa ilani zake na baada ya hapo tunawachunguza wagombea ambao ni watekelezaji wa ilani hizo. Hapo tutaweza kutoka tulipo kwenda mbele, kama hatukukosea hapo.
Maisha ya watanzania yamebadilika katika mambo mengi. Mengi sana. Tanzania yenyewe imebadilika. Imebadilika sana. Taja jambo lolote. Ukilipima jinsi lilivyokuwa 1961/4 na kulilinganisha na sasa, utaona mabadiliko makubwa. Nitataja machache:
1) Tumetengeneza Tanzania. Zamani tulikuwa makabira. Watawala wetu wakatuunga katika mataifa ambayo tuliyakomboa kwa kuwaondoa watawala. Baadaye Tukaunganisha Tanganyika na Zanzibar na kupata Tanzania. Kuna watu wanahoji uhalali wa Tanzania lakini hawahoji uhalali wa Tanganyika. Tofauti ni kuwa Tanganyika iliundwa na wakoloni lakini Tanzania tumeiunda sisi watanzania.
=Tanganyika ilipatia uhuru wake mwaka 1961 Na kuungana na Zanzibar 1964 na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
2) Nakumbuka mwaka 1962 alikuja Chifu wa eneo letu (Omukama Lutinwa) shuleni Katarabuga Wilayani Missenyi. Wanafunzi tulijikusanya na kupiga magoti katika uwanja na walimu wakajipanga kumsalimia wakiwa wameinama. Salamu yenyewe inasema Uinulimwe muweza-Habuka Lugaba. Inadhalilisha. Ukilinganisha na sasa ona kwenye mitandao hii tunavyomchambua Kikwete. Hata kuandika neon Kikwete bila kuweka neno Mheshimiwa, au Mtukufu, enzi hizo ningekamatwa.
3) Myaka hiyo ya mwanzo wa uhuru Kupiga mswaki asubuhi lilikuwa somo darasani. Kuvaa nguo ya ndani kabla ya kaptura ilikuwa hadithi au watoto wa matajiri na tulikuwa tunaonyeshana –fulani anavaa chupi. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema alivaa nguo akiwa na myaka 12 wakati akienda shule. Tulitembea kilomita 10 kuifuata shule ya dhehebu letu na kuipita shule isiyo ya dhehebu letu. Ni tofauti na sasa. Mswaki ni wazazi wanamfundisha mtoto nyumbani, nk nk nk. Tukiziangalia idadi ya shule karibu kila kijiji kina shule ya msingi, kila kata ina shule ya sekondari kila wilaya ina chuo cha aina Fulani.
4) Mpaka 1980 nadhani; magazeti yalikuwa ni UHURU na Daily News na mfanyakazi (Gazeti la NUTA). Gazeti huru la kwanza lilikuwa Majira. Sasa tunachagua kusoma hili na kuliacha lile. Radio pekee ilikuwa RTD (Radio Tanzania Dar Es Salaam). Sasa karibu kila mkoa una vituo vitatu mpaka vine.
5) Usafiri wa kawaida kutoka mathalan Kijijini kwetu Bwanjai kuja Bukoba mjini kilomita 25 usafiri ilikuwa ni kutembea kwa mguu au baiskeri.
6) Mpaka 1977 Mtu ukipanda gari Tukuyu asubuhi ulikuwa ukifika Dar Es Salaam kesho yake saa nne. Hapo mmetembea mchana kutwa na usiku kucha.
7) Kuna tunaokumbuka wakati ule tunachagua kati ya Nyerere na bure. Wabunge walikuwa wanatembea pamoja kwenye gari. Wakifika kila mmoja anajieleza halafu wanaondoka wote. Mwaka huu tunauamuzi kati ya watu wanane.
Hata kwa hayo machache; yasiyo na yaliyo ya msingi nitamshangaa mtu anayewakubalia wanaosema Vyama vilivyopigania uhuru havijafanya lolote. Sitavishangaa vyama ila wanaovikubalia. Sitavishangaa vyama wala viongozi wake Maana mkapa alishalimaliza siku ya ufunguzi wa kampeni.
Elisa Muhingo
0767 187 507
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments